Wasanii na viongozi wa WCB waalikwa nyumbani kwa rais mtaafu Jakaya Kikwete

Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete Jumatano hii aliwaalika wasanii wa label ya WCB pamoja na viongozi nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana.

JK ambaye ni mmoja kati ya marais ambaye amesupport sana wasanii wa muziki nchini, aliwaalika wasanii hao nyumbani kwake na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu muziki wao.

Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam alimshukuru rais huyo kwa kuwaalika nyumbani kwake na kuzungumza nao mawili matatu kuhusu muziki.

“Former President JM Kikwete and Former First Lady Mama Salma Kikwete. Asanteni kwa mwaliko wenu!! Allah awape afya njema,” Sallam aliandika instagram.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa ndio viongozi wetu wa Chama Tawala CCM, hebu fikiria mwenyewe, kiongozi mstaafu mzima kama huyu badala ya kwenda kuwajulia hali wahanga wa tetemeko la ardhi pale kwenye mikoa ya Kagera na Mwanza. Yeye anawaalika wanamuziki wa Bongo Fleva na kula nao Lunch duh. Kwani ingekuwa busara zaidi kama angekula Lunch na wale wahanga wa tetemeko la ardhi. Kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake. Ama hilo nalo alikuwa anasubiri apate ushauri????? Mbona ni common sense ys kawaida kutoka kichwani.

    ReplyDelete
  2. Acha ushabiki wa kisiasa na NONGWA, unajua walipata lini mwaliko huo? hawa ni vijana wetu na kuwa karibu nao ni muhimu. Angekuwa Lowasa kakutana nao ungeyasema haya? acha mawazo finyu na dhaifu, waliopata janga kuna mamlakana watu ambao wamepewa majukumu ya kufanya, hivi watu wote wakiamua kwenda mkoani Kagera kutatosha huko? siasa chafu na zenye dalili ya wivu na roho mbaya ziacheni, mbona wote ni Watanzania? ingekuwa kuwakaribisha wasanii wageni toka nje ya nchi uenda mawazo yako yangekuwa na mashiko, unachokifanya wewe unaendeleza itikadi yenu ya ubaguzi wa watu na siasa za nguvu za giza.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad