Wazanzibar Waisifia Hotuba ya Rais Magufuli

Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wamempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kutoa hotuba waliyoiita ‘safi’ inayosadifu hali ya maisha ya watanzania.

Kwa siku na nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa Zanzibar walisema kuwa hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa katika mkutano wa kutoa shukrani baada ya uchaguzi uliopita, imejenga imani kubwa kwa maendeleo na wananchi sambamba na kukemea suala la ubaguzi miongoni mwa wananchi na viongozi.

Moja kati ya wakati wa Zanzibar waliweza kutoa maoni tofauti tofauti kuhusiana na hotuba hiyo.

“Rais Magufuli alizungumzia vizuri suala la amani, halafu vilevile bila amani usingeweza kuja kunihoji hapa kwa hiyo amani ndio kila kitu,” alisema mkazi mmoja wa Zanzibar.

“Kwanza nampongeza mheshimiwa rais kwasababu hotuba yake imetufanya sisi vijana tuamke na tufanye kazi na sio kukaa maskani kama unavyotuona hapa,” alisema kijana mmoja.

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli alisisitiza zaidi suala la maendeleo.

“Tunataka maendeleo, na mimi niwaombe ndugu zangu watanzania wote, lengo letu kubwa liwe maendeleo kwa watanzania, maendeleo kwa wazanzibar, maendeleo kwa wapemba, tupeleke Tanzania yetu mbele,tupeleke Zanzibar yetu mbele, vyama tuweke pembeni,” alisema.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wanzanzibar gani hao?
    Fyuuuuuuu
    Wazanzibari tunatamba Zanzibar yenye mamlaka kamili
    Fyuu sheni ufundishwe kutawala na rais wa tanganyika wakati nawe u rais
    Fyuuuuu

    ReplyDelete
  2. Wanzanzibar gani hao?
    Fyuuuuuuu
    Wazanzibari tunataka Zanzibar yenye mamlaka kamili
    Fyuu sheni ufundishwe kutawala na rais wa tanganyika wakati nawe u rais wa Zanzibar ati
    Na kuambiwa Nani apate tunzo
    Jumbe mpk kafa hata mtaa kuitwa jina lake kisa alikuwa anatetea Zanzibar kuwa Huru
    Muungano wa kulazimishana hatutaki
    Kura ya maoni tunaitaka
    Fyuuuuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtachonga sana wazenji lakini Magu ndo habari ya mujini funga muziki

      Delete
  3. Kaisifia jecha pekee yake hata shein hajaipenda kuitwa mpole aongeze ukali
    Kwani rais wa Zanzibar ni mkuu wa mkoa wa waziri wa Tanganyika ?

    ReplyDelete
  4. Maendeleo ya subiri sana brother another fifty years to come utayapata serikali ile ile mfumo ule ule just kubadilisha maneno ya kutishana tu hamna lolote uta subiri sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hama nchi mnafiki wewe maendeleo yanaanzia kwako utakuta mwenyewe unamiaka hamsini kiti cha kukalia nyumbani kwako huna unataka uletewe na serikali

      Delete
  5. Tuko wazanzibar wengi tunokubaliana na maneno ya rais kwani kasema ukweli kabisa. Ni wakati wa kujenga Tanzania yetu tuachane na hii fyoko fyoko.

    ReplyDelete
  6. walioipongeza ni VILAZA, alifikiri wapemba ni VILAZA VYA CHATO?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad