SERIKALI Mkoa wa Dodoma imesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atahamia rasmi mkoani humo mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge vinavyoanza wiki ijayo, Septemba 6.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema baada ya kufika Dodoma, ataanza kuratibu utaratibu wa wizara mbalimbali kuhamia katika Makao Makuu hayo ya nchi.
Pamoja na hayo Jeshi la Polisi limejipanga kuongeza vituo vya Polisi ili kuimarisha ulinzi wakati serikali itakapohamia na hakuna mwananchi atakayenyang’anywa ardhi yake kwa sababu yoyote ile.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Rugimbana alisema kama mkoa walishauri ujio huo ufanyike mara baada ya kikao cha Bunge na Waziri Mkuu ameridhia suala hilo.
Alisema Waziri Mkuu atakuwa Mratibu wa wizara zote kuhamia Dodoma na kazi hiyo ataianza rasmi mara baada ya kuwasili mkoani humo.
Alisema maandalizi yanaendelea vizuri na ukarabati wa nyumba ya Waziri Mkuu umefikia asilimia 90.
Alisema Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christine Mndeme aliyekutana na makundi mbalimbali kwa ajili ya mapokezi ya Waziri Mkuu.
“Awali tulisema atakuja Septemba Mosi lakini baada ya kushauriana tumeona aje mara baada ya vikao vya Bunge kwani pilikapilika nyingi zitakuwa zimepungua, kama serikali ikiamua kuja leo tutaipokea kwani maandalizi ya serikali kuja Dodoma yamekamilika kwa asilimia 70,” alisema.
Kwanini wasishauriane kabla ya matamko yao kuwa atahamia sep 1?
ReplyDeleteKaribu sana Mh Majaliwa. Dodoma mnakarishwa waheshimiwa kwa nyoyo zetu kunjufu na tuaahidi kushirikiana nanyi kwa hali na Mali.. Milango yetu iko wazi na familia zetu zinafuraha kuona ndugu zetu. mnakuja kuungana nasi katika ushirikiano wa maisha hapa kwetu na ni kwenu karibuni sana na wakati wowwote saa yoyote.Jihisini mko nyumbani.. Karibuni Sana.
ReplyDeleteKama kaiwaida ya awamu ya tano kukurupuka na kuropoka kabla ya kufikiri
ReplyDeleteFyuuuuuuu
mtaumbuka fikirieni kwanza kabla ya kusema
wajinga na wapumbavu uta wajuwa tuuuu
vishindo vyote pesa ya huhamia hamna
Hata ROM haikujengwa kwa mwaka
Mfupa aliushindwa fisi mbwa atauweza ????
Kuhamisha makao makuu yanataka pesa na plan
mmetubia pesa zetu miaka yote
watu wanna nyumba dar na Dodoma
fyuuuuuuu
Tanzania ni nchi pekee duniani yenye makao makuu mawili
Pamoja na kuwa nchi maskini duniani