Waziri Mkuu: Serikali Haijashindwa Kuongoza Nchi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo macho, haijalala na haijashindwa kuongoza nchi bali imejipanga  kuliongoza Taifa kwa mafanikio makubwa.

"Serikali haijashindwa kuongoza nchi. Nataka niwahakikishie waheshimiwa Wabunge na wananchi wote kwamba tutaongoza nchi hii kwa mafanikio makubwa na kazi hiyo imeanza kwa marekebisho makubwa kwa maeneo ambayo tunadhani yatafanya Taifa hili liweze kupata mafanikio makubwa,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Septemba 8, 2016) Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Bw. Freeman Mbowe, ambaye alitaka kufahamu Serikali ina mkakati gani wa kunusuru mdororo wa uchumi uliopo nchini.

Bw. Mbowe alidai kwamba hali ya uchumi imeshuka na kwa mujibu wa taarifa za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) uagizaji wa bidhaa kutoka nje umepungua, uuzaji wa bidhaa nje ya nchi na sekta ya ujenzi imesimama hali inayoashiria kudorora kwa uchumi.

Kuhusu suala la kupungua kwa mizigo katika bandari na vituo vya forodha, Waziri Mkuu amesema usafirishaji wa mizigo kwa njia ya bahari umeshuka duniani kote kwa sababu ya kushuka kwa hali ya uchumi kutokana na kuporomoka kwa bei ya mafuta na gesi.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema tayari wafanyabiashara wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wameihakikishia Serikali kwamba mizigo yao yote itakuwa inapitia Bandari ya Dar es Salaam hasa kwa mkakati wa pamoja wa ujenzi wa reli ya standard gauge inayoanzia Dar es Salaam-Tabora - Isaka.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha inaendelea kuimarisha amani na ulinzi kwenye maeneo yote nchini na kwamba vyombo vya dola viko macho. “Watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu yakiwemo mauaji watakamatwa popote walipo na kuchukuliwa hatua za kisheria,; amesema.

Amesema hatua hiyo inatokana na matukio ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni ambapo raia wasiokuwa na hatia na askari waliuawa katika maeneo ya Vikindu mkoani Pwani, Tanga na Mwanza. Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani

Katika swali lake, Bw. Ngonyani alitaka kujua ya Serikali kuhusu  kukomesha mauaji hayo, yanayotokea kwa watu wasio na hatia pamoja na askari, ambapo Waziri Mkuu, alitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wananchi na familia, ambazo ndugu zao walipoteza maisha katika mauaji hayo.

Pia ametoa wito kwa Watanzania wote kuhakikisha wanawafichua watu ambao wanawatilia shaka na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili waweze kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua

Habari na Ofisi ya Waziri Mkuu
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmmh si tupooo yetu machooo...

    ReplyDelete
  2. Hongera shemeji wa kikwete
    Mtoto wa mama mkubwa na mdogo mwa salma
    Chezea ccm wewe
    Tangu shemeji atumbuliwa
    Pole Mbowe to

    ReplyDelete
  3. Pamoja na kufanya kazi nzuri awamu Tano ina kasoro kubwa ambayo huenda ikaigharimu Tanzania
    Uhuru wa watu kuikosoa serikali
    Waachieni watu waikosowe serikali Nina Imani kabisa 90%
    Ya ukosowaji ni kweli
    Nchi nyingi duniani zillingia kwenye migogoro Kama hii
    Wakikosoa wajibuni kwa hoja
    Pili kukurupuka kila kukicha na agenda mpya nafikiri tujirekebishe
    Tulianza elimu
    Hili suala si dogo
    Madawati
    Waalimu
    Shule zenyewe
    Je tumefanikiwa kwa asilimia ngapi ?
    Ulipaji kodi Watanzania wote wanajua umuhimu wa kulipa kodi
    Hangii akilini kama mteja nisipopata lisiti nitashistakiwa
    La kuhamia Dodoma linachekesha sana
    Makao si kuhamia kwenye majengo
    Mabolozi wote na ofisi za kimataifa zipo dar
    Miundo mbinu yote ipo dar
    Tusikurupuke
    Mawaziri msikubali kila kitu
    Magu ni binadam Kama Watanzania wengine


    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad