Wema Sepetu na Idris Sultani Bado Ngoma Nzito...Ampigia Chapuo Kevin Hart MTV Mama Badala ya Idriss

Adui yako muombee njaa – Wema Sepetu na Idrs Sultan ngoma bado ngumu.

Wema amepigilia msumari wa moto kwa kupost picha ya mchekeshaji wa Marekani, Kevin Hart ambaye anawania nafasi ya kuhost kwenye tuzo za MTV MAMA mwaka huu na Idris Sultan kama mwanaunme anayempenda #MCM (Man Crush Monday. “MCM….😏😏😏,” ameandika Wema kwenye picha hiyo.

Kitendo hicho cha madam Sepetunga kimetafsiriwa ni kama anampigia chapuo mchekeshaji huyo wa Marekani kushinda nafasi hiyo na kumponda kiaina ex wake, Idris.

Hivi karibuni wawili hao walionekana mahusiano yao kuingia doa na Idris akijikuta akiifunga akaunti yake ya Instagram kwa muda baada ya kuambulia matusi kutoka kwa watu wanaojiita ni Team Wema.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. bongo bado sana,yaani mnaombeana njaa wenyewe kwa wenyewe,pumbafu sana.Ndio maana wakenya wanatucheka.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad