ZITTO Kabwe Afunguka Kuhusu Utafiti wa Twaweza Kuhusu Imani Waliyonayo Wananchi Kwa Rais Magufuli

Kura za Maoni zilizotolewa na TWAWEZA zinaibua maneno ambayo unashangaa kuyasikia kwa wasomi, wengine maprofesa. Kwangu mimi naona masuala 2 muhimu


  • Matokeo yanaonyesha IMANI kubwa ambayo wananchi wanayo kwa Rais Magufuli. Hata hivyo IMANI hiyo inakuja na wajibu mkubwa sana na Rais asitumie vibaya imani hiyo. Kiongozi mwenye busara hawezi kutumia imani hii kwa kukandamiza demokrasia na kukanyaga Katiba. 
  • Matokeo pia yanaonyesha kuwa Wabunge na Madiwani kwa kiasi kikubwa wana IMANI ya wananchi wao wanaowawakilisha. Huu ni wajibu na fursa kwa Wabunge wa Upinzani kuonyesha uongozi mahiri wenye kutoa majawabu ya changamoto za wananchi kwenye maeneo yanayoongozwa na Vyama vya Upinzani.


Tujifunze kukubali tusiyopenda kuyasikia. Wakati tunapambana vita adhimu sana dhidi ya Udikteta Mamboleo unaonyemelea nchi yetu, pia kwa nguvu hizo hizo tuonyeshe tofauti ya kiuongozi katika Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji tunayoongoza

By Zitto Kabwe

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿😜🇹🇿🇹🇿😜😘😘🍻🍻🍻🍻🍻🍻

    ReplyDelete
  2. Wewe Zitto ndo kina 4% wakati wenzio maisha yanasonga mbele umeng'ang'ania kukandamiza demokrasia na kukanyaga Katiba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haka kajamaaaaa kako so miserable duh

      Delete
  3. Namuunga mkono Zitto.nyinyi wengi mnliochangia hamna elimu za juu. Kazi zenu ni kububuja maneno tu. Maprofesa na wasomi wengi vilaza. Wanadegree za karatasi kichwani kutupu. Pia hawana uhuru, mawazo binafsi ya kuiendeleza wala muendeleza nchi.wanapewa mishahara bure.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad