Zombe Aachiwa Huru, Mshirika Wake Ahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa

Mahakama ya Rufaa imemhukumu aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni kunyongwa hadi kufa katika kesi ya vifo vya wafanyabiashara wa madini iliyokuwa ikimkabili yeye pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe na maofisa wenzake wawili.

Katika hukumu hiyo, Zombe na maafisa wengine wawili wameachiwa baada ya kushinda rufani hiyo dhidi yao.

Hukumu hiyo imehitimisha mvutano wa muda mrefu wa kisheria kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na maofisa hao kwani baada ya kimya kirefu hukumu hiyo imetolewa.

Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa ni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mratibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Hukumu hiyo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu, wakiwamo ndugu wa marehemu hao, wanasheria na jamii kwa jumla baada ya miezi minne, majuma mawili na siku mbili, tangu rufaa iliposikilizwa.

DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyowaachia huru Zombe na wenzake wanane katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wawili wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva wa teksi, mkazi wa Dar es Salaam.

Katika kesi ya msingi, Zombe na wenzake walidaiwa kuwaua kwa kukusudia wafanyabiashara Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na Juma Ndugu, aliyekuwa dereva wa teksi wa Manzese.

Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, mwaka 2006, katika msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini.

Agosti 17, 2009, Mahakama Kuu iliwaachia huru washtakiwa hao ikisema baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za mawakili wa pande zote iliridhika kuwa hawakuwa na hatia ya mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Badala ya kosa la mauaji ambalo adhabu yake ni kunyongwa hadi kufaa, DPP aliiomba Mahakama imtie hatiani Zombe kwa kosa la kuwalinda wahalifu, ambao adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka saba jela.

Wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Timon Vitalis alidai DPP alifikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa hakuna ushahidi wa kumtia hatiani Zombe kwa kosa la mauaji.

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mh!! at last hukumu imetoka da!!! wale watu waliuawa bila hatia masikini kisa mali zao!! hiyo ndiyo iliyokuwa dora badala ya kulinda inakuangamiza mwe!!! sasa huyo aliyehukumiwa kifo mbona hamjafafanua yeye alihusikaje haswa? au ndiyo aliyewalipua za kisogo!!!Ni vyema dora kulinda jamii na siyo kuipoteza!!! sijui ni vipi mama wa wale watu aliumia!!! only God knows about that....

    ReplyDelete
  2. Zombe aachiwa huru mshirika wake anyongwa jamani naomba tafsiri ya mshirika ninavyojua ni muumgano wa kushiriki kufanya kitu pamoja sasa inakuwaje mshirika ananyongwa na mwingine anaachiwa huru au ndio demokrasi mwandishi yuko huru kuandika habari tofauti na mantiki ya mahakama kumwachia huru mshitakiwa baada yakuonekana hakushiriki ktk mauaji lakini bado mwandishi anamwita mshiriki

    ReplyDelete
  3. Hii ndo siasa ya Tanzania.hapa unaona wazi sheria na siass zimeingiliana.Hatutakuwa salama Tanzania kama wstu wa usalama pia wanachezea usslama hii insonrkana wazi. Mchezo mchafu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad