Alikiba Ana Mziki Mzuri Lakini Kuna Walakini Mahali...Hivi Hana Timu ya Kuhakikisha Kila Kitu Kipo Sawa?

Ule usemi wa kwenye miti hakuna wajenzi nimeliona kwenye hiyo Show ya Mombasa hasa baada ya Ali Kiba kuhojiwa na kipindi cha Mseto... kwa kweli huyu msanii anahitaji Management. Anajisikia sana anategemea mashabiki sana anasahau hata mitume walisalitiwa na watu "Eti sallam alikuwa backstage" Swali la kujiuliza hapo timu yake ilikuwa inafanya nini mpaka Sallam Akafanya yake kuzima mziki?

Huyu jamaa hayupo kibiashara amejidhalilisha sana kwa kuonyesha team ya Diamond ipo vizuri sana kiasi cha kumdhalilisha. Hivi huyo msanii wa Marekani na Alikiba mbona wapo sawa tu? Hakupaswa kurudi jukwaani kuimba.

Ni muda umefika akapata management amabayo inajua ataongea nini atavaa nini alale wapi. Na kama anayo management awafute kazi. Nadhani Alikiba anahitaji msaada haiwezekani aende Kenya bila mtu backstage.

By Pascal Ndege

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wewe umesema!! anahitaji management. kama ipo basi imekufa.!!

    ReplyDelete
  2. wacheni uppuzi leave the guy alone mbona munaropoka ovyo hapiti mpizani hata iwe vipi salam salam sasa ndio mumemesema nini tumfanye nini huyo salam na kwanza kilichomleta mombasa ni kipi na kama kweli alikuwa ana kazi basi iweeje wakati uwe huo huo kwanini hakuja kabla wacheni kukuza chuki king is kiba will remain the same sauti yake mashallah so nyie mlalamike halafu usiku mukalale

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad