Aliyepigwa na Walimu Mbeya aeleza kwanini hakwenda Hospitali

Jina lake ni Sebastian Chinguku mwanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya Day kidato cha tatu ambae video yake ya kupigwa fimbo mateke na makofi na Walimu ilisambaa sana kwenye mitandao na imekua gumzo mpaka viongozi wa Serikali ikiwemo Mawaziri kuingilia kati.

Anachokisema leo Sebastian kwenye AyoTV ni kwamba hakwenda Hospitali baada ya kuumizwa na kipigo cha Walimu sababu aliogopa angeulizwa PF3 lakini pia baada ya kipigo alishindwa kuendelea kwenda shule sababu ya maumivu na nguo za shule zilichanika akipigwa.


‘Baada ya tukio walimu waliniuliza mimi kama mimi nafanyaje, nikawaambia mimi nasamehe hili swala baada ya kuona Walimu wameshachukulia mimi ndio mwenye matatizo, nilihofia kufukuzwa shule moja kwa moja maana kosa langu niliambiwa ni kosa la kupiga Walimu‘ anasema Sebastian

‘Baada ya hapo sikuona haja ya kwenda Polisi au kulifikisha hilo swala popote kwengine kwasababu nilishawasamehe tarehe 28 September, nikabaki nyumbani tu baada ya tukio nikawa nauguzwa na pacha wangu ambaye ni mdogo wangu, Baba yuko kikazi Mbozi na mama yuko Dar anauguza… shule sikwenda toka September 28‘ – Sebastian


Sebastian anasema chanzo cha kupigwa na Mwalimu ni kutokufanya kazi iliyotolewa na Mwalimu darasani siku ya Jumatatu
 ‘Sikuweza kuifanya sababu sikwenda shule Jumatatu nilikua naumwa, nilipokwenda Jumatano nikakuta adhabu inatolewa, nikamuelezea Mwalimu kuwa nilikua naumwa lakini hakunisikiliza hivyo nikakubali kuadhibiwa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad