Belle 9 Aupiga Vijembe Mziki wa Singeli..Adai ni wa Kupita Hawezi Jiingiza Huko

Belle 9 amesema hafikirii kabisa kufanya muziki wa
Singeli.

Muimbaji huyo wa R&B amesema huo ni muziki wa
kupita na katu hauwezi kudumu.

Alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa swali na mtangazaji
iwapo atafanya muziki huo mashabiki wakimtaka.

“Sitegemei,” alisema Belle9

“Hata kama nitafanya, sitofanya kama release song sababu
Singeli ni muziki fulani hivi ambao unapita, ni bubble gum
music. Sasa hivi watu wanaushabikia lakini itafika time
utapita, sio muziki wa kustick.”

JE UNAKUBALIANA NAYE?
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad