CHADEMA yapinga kununuliwa na Lowassa, yashindwa kuzungumzia tuhuma za ufisadi.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema ni uongo na ni propaganda za wapinzani wao kwamba Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alimhonga Mwenyekiti Freeman Mbowe ili kupata nafasi ya kugombea urais mwaka 2015.

Dkt.  Mashinji ameyasema hayo katika kipindi cha Kikaangoni  kinachorushwa na kituo cha EATV kupitia ukurasa wa facebook ambapo wananchi walikuwa wakimuuliza maswali ya papo kwa papo naye anayajibu.

“Si kweli kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe alimhonga Lowassa ili agombee urais kupitia CHADEMA , ni propaganda zinazoenezwa na wapinzani wetu ili kuwadanganya wananchi” Amesema Dkt. Mashinji.

Amesema Lowassa alijiunga na CHADEMA kwa njia halali kwa mujibu wa taratibu za chama, na maamuzi ya kumteua kugombea urais yalifanywa na vikao halali kuanzia ngazi ya Kamati Kuu hadi Mkutano Mkuu.

Kuhusu sababu za CHADEMA kumkaribisha Lowassa licha ya kumtaja miaka mingi kuwa alihusika na ufisadi, Dkt Mashinji, hakutaka kulifafanua kwa undani, lakini aliishia kusema kuwa wao walijiridhisha kuwa hakuwa na hatia yoyote na kwamba kama kweli alikuwa ni fisadi, basi vyombo vya dola vingemchukulia hatua.

"Kama mtu kweli alikuwa ni fisadi, kwanini hakuwahi kuchukuliwa hatua, hata kufikishwa mahakamani?, nadhani hilo tuliache" Alisema kwa ufupi Dkt Mashinji.

Aidha Dkt. Mashinji amewataka watanzania na wapenzi wa CHADEMA kufahamu kwamba chama hicho hakipo kimya bali kinaendelea na mikakati ya kuhakikisha kwamba kinawafikia watanzania kwa kuwatetea kwa kila hali kutokana na mambo yanayoendelea nchini.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. CHADEMA ndio mliokuwa mnapiga kelele ya kwamba Lowasa ni fisadi,na kwamba anahusika na RICHMOND kwa 100%,Kinachoshangaza mlimsafishaje mpaka mkampa nafasi ya kugombea urais.Muwe wakweli,nyie mlijua Lowasa alikuwa na nguvu nje na ndani ya CCM,(kweli tupu),Na kwa kuwa mlikuwa na uchu wa madaraka mliamini akija CHADEMA wale Wapenzi wake wote na hata waliokuwa CCM wangempa ushirikiano hata nje ya CCM.Swala la kwa nini hakushtakiwa kama ni fisadi,labda tuambie kabla ya JPJM ni wangapi walishastakiwa kwa ufisadi na walifanywa nini?Wakati mwingine mnatakiwa mjiongeze kabla ya kuhoji mambo sio kuropoka tu ili mradi uonekane umeongea.Hivi ni kigezo gani kiliwafanya mumkubali na mumpe nafasi kubwa Lowasa,kiongozi ambaye alijiuzulu kwa kashfa akiwa waziri mkuu na wote mkiwa bungeni mliridhia kujiuzulu kwake?Kubalini mlikosea sana,na pengine mlitakiwa mumtumie lowasa kwenye kampeni tu na sio kumpa nafasi kubwa vile na urais akabaki Dr.Slaa pengine TZ ingekuwa chini ya CHADEMA sasa hivi.MMELIKOROGA,Mlinywe tu.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  2. Hii mpya,SIO MBOWE ALIMHONGA LOWASA,ni LOWASA ALIMNUNUA MBOWE.(Inasemekana lakini,)

    ReplyDelete
  3. CHADEMA SASA HIVI INATAKIWA NGUVU ZA ZIADA KUTULUBUNI TENA,MAANA HII KASI YA HUYU RAIS WA AWAMU YA TANO SIO MCHEZO.

    ReplyDelete
  4. Waambieni ingawaje ni nusu viziwi watasikia.
    Wapinzani hapa nchini ni sawa na ukoma. Wanachelewesha umoja na maendeleo yetu.

    ReplyDelete
  5. Jamani mbona mnatoa Siri za Watu?? Au mnataka kuwafikisha kubaya. Mimi sitaki kuwa shahidi... Aka mimi simo.. Muulizeni mwenyewe. Hata kama niliona.

    ReplyDelete
  6. Jamani mbona mnatoa Siri za Watu?? Au mnataka kuwafikisha kubaya. Mimi sitaki kuwa shahidi... Aka mimi simo.. Muulizeni mwenyewe. Hata kama niliona.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad