Mara nyingi wasanii wa nje wanapokuja kwenye show Afrika, hupenda kujichanganya na wasanii wanaotangulia kwenye show yake na kuchukua selfie na vitu kama hivyo. Lakini kwenye tamasha la Mombasa Rocks lililofanyika Oktaba 8 mjini Mombasa ambalo Chris Brown alitumbuiza, hakuna picha yeyote iliyoonekana akiwa na wasanii waliomsindikiza – Wizkid, Vanessa Mdee na Alikiba.
Kwa mujibu wa Vanessa, Chris hakuwa kabisa kwenye mood katika siku hiyo nzima na hakutaka kuongea na mtu. “To be honest, Breezy was not in a good mood,” Vanessa aliwaambia watangazaji wa XXL ya Clouds FM Jumatano hii.
“Tangia tumefika hadi tumeondoka hata ku.. sijui labda mazingira yalikuwa hayamfurahishi. Amepokelewa vizuri sana, sijui, alikuwa hana mood ya kusocialize na mtu yoyote,” ameongeza.
Kwa upande mwingine Vanessa alizungumzia sakala ya Alikiba kuzimiwa mic kwenye show hiyo.
“Mimi nilikuwa namsubiria Alikiba kama wewe ulivyokuwa unamsubiria, mimi nilikuwa nataka kuona show yake maana Mombasa wanamkubali sana but kilichotokea ni kwamba nadhani muda ulikuwa umeshatimia na Chis Brown muda wake wa kupanda stejini ulikuwa umeshafika, so that’s what happened, that’s what I know hayo mengine mimi siyajui,” alisisitiza.
“Halafu kibaya ni kwamba walikuwa wamesubiri kwa muda sana, kulikuwa na delay baada ya performance yangu mpaka alipopanda Wizkid, long time walikuwa wamesubiri na yeye [Chris Brown] alikuwa ameshaanza [kulalamika], ni kama nilivyosema alikuwa in a very bad mood. Kwahiyo walikuwa wanajaribu kumridhisha yeye ili apande muda ambao anataka yeye.”
Chris Brown Hakuwa Kwenye Mood na Hakutaka Kuongea na Mtu – Vanessa Mdee
3
October 12, 2016
Tags
Fuckin'baby crap waafrika huko nyumbani kuwababaikia waamerika weusi wakati wengi wao hawana mpango kabisa na sisi waafrika KALAGA BAO
ReplyDeleteKweli kabisa uyasemayo. Wanapenda sana kujikomba. Ati Cris hakuwana moody mzuri. Yeye si analipwa au hiyo shoo kafanya bure. Pumbavu yake. Ali kiba kwangu ni bora mara elfu kuliko yy.kwanza ni mu Africa mwenzetu raha na tabu zetu anazipata kama sisi. Hao wamarekani weusi wengi wao hawawapendi wa Africa. Ila sie ndio wajinga kwa kujikomba kwa kila mtu ambao sio mu Africa na ndio maana tunadharaulika duniani kote
DeleteWord! we despise our own and bad enough;WE DESPISE OUR OWN SELVES. So nani atakuheshimu na kukuthamini kama hujitathimini wala kuthamini vyako? CB awe kwenye mood asiwe kwenye mood to hell! mood yake isingewapa shida kama si kumshobokea, Be professionals.handle yourselves with dignity&class and you will earn it. vinginevo mnatudhalilisha sote kama waafrika kwa shobo zenu.
ReplyDelete