wa
Mhe Hapi amesema, hatua ya kuwaweka ndani watendaji hao na mkandarasi itawakumbusha juu ya utekeleza wa miradi wanayotakiwa kusimamia na nini majukumu yao kwa wananchi kwa madai kuwa uzembe umekithiri.
“Ofisi inapesa kwa miaka miwili sasa ya kujenga Zahanati lakini wamekalia tu pesa hizo tangu 2014, pia miradi ya barabara na kushindwa kuweka polisi jamii ndani ya kata hiyo licha ya kupewa maagizo kwa miezi 3 sasa hii ni dharau kwangu na Rais aliye nituma” amesema
Aidha Hapi amewataka watendani wote wa kata na maafisa ugani waliopo katika wilaya hiyo kujiengua kwenye nyadhifa zao endapo wanaona hawawezi kuendana na kasi inayotakiwa na serikali ya awamu ya tano.
Lakini pia amemtaka mkuu wa kituo cha polisi wa manispaa ya kinondoni kuwakamata watendaji kata wote ambao hawajaunda vikundi shirikishi na kuwaweka ndani kwa muda wa masaa 24 ili waweze kujieleza.
Sawa sawa Hapi. Mwamko na uwamshaji ni Jukumu lako. Na wasipoelekea wanarudisha Pesa walizo kunywa na Tenda tunatangaza Upya. Mchezo na ujanja ujanja hatutaki katika Awamu yetu hii ya Tano. Hapa Kazi Tu. Siyo siasa siasa nyingi. Hatutaki hilo!!!!
ReplyDelete