Dc Makete Atoa Maagizo Mazito Kwa Walimu Wanaotembea Na Wanafunzi

Katika kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, wanafunzi wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kusoma kwa bidii kwa kuwa taifa linawategemea ikiwemo kuja kushika nyadhifa mbalimbali baada ya kuhitimu masomo yao

Kauli hiyo imetolewa jana na Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessi yaliyoadhimishwa kiwilaya katika shule ya Sekondari Lupalilo

Aidha Mkuu huyo ametoa Onyo kali kwa walimu wote wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi na kusema sheria zipo wazi kwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua, huku akiwataka wanaofanya hivyo kama wapo kuacha vitendo hivyo mara moja

Naye diwani wa kata ya Tandala Mh Egnatio Mtawa ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete akishukuru kwa hotuba ya mgeni rasmi amesisitiza maagizo hayo wahusika wayafanyie kazi ili kuepusha madahara yatakayoweza kujitokeza endapo maagizo hayo yatapuuzwa

Awali katika maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine wanafunzi wa shule ya sekondari Lupalilo wamepatiwa elimu ya Virusi vya Ukimwi na UKIMWI kazi iliyofanywa na Mratibu wa Ukimwi sekta zote Wilaya ya Makete Bi Ester Lamosai ambapo pamoja na mambo mengine amemueleza mgeni rasmi jinsi ambavyo shule nyingi hazipo salama kwa sasa
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ph.D. Zingine zinatia wasiwasi tena za chemistry or fisikia au hesabu
    Mtu waziri ana muda gani kwenda maabara kufanya utafiti
    Tanzania hiyo na CCM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad