Diamond Akiri Mimba Ya Mobeto Kuharibika


BAADA ya ukimya wa muda mrefu kutawala kuhusu ujauzito alionao mrembo anayesumbua Bongo, Hamisa Mobeto, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibuka na kukiri kuwa mimba ya mrembo huyo imeharibika.

Diamond aliyekuwa akitajwa kuwa mhusika wa kiumbe hicho, alifunguka hayo kupitia Kipindi cha D’ Wikend Chart kinachorushwa na Runinga ya Clouds mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine aliyozungumza, alikanusha taarifa za yeye kuwa mhusika lakini akakiri kwamba mrembo huyo alikuwa mjauzito na sasa mimba imeharibika.

“Mimi mwenyewe nilikuwa sijui kama ana mimba lakini ndiyo hivyo tena imeharibika so yupo kwenye wakati mgumu. Tumpe pole na tumpe pole pia aliyekuwa mhusika wa kiumbe hicho.

Mimi si mhusika bwana, hata wakati tunashuti naye Salome nilikuwa sijui kama ni mjamzito lakini ndiyo hivyo kwa sasa hatuna budi kumuombea arudi katika hali yake ya kawaida,” alisikika Diamond. Ijumaa Wikienda lilimvutia waya Mobeto ili kuweza kumsikia kama ana lolote kuhusu ishu hiyo, simu yake iliita bila majibu.

Ujauzito wa Mobeto ulikuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi waliamini mhusika ni Diamond kitendo ambacho kilisababisha maneno kumfikia mpenzi wa staa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na kutibua hali ya hewa lakini kwa sasa mambo yako shwari baada ya Zari kuelewa kwamba Mobeto hana madhara.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmh! Huyu bibi-bomba Mganda inaelekea ni 'kigagula'..... mbona mahasimu wake kila wakishika mimba zinaharibika?? Yeye anafyatua tu asubuhi na jioni.....nina wasiwasi nae........

    ReplyDelete
  2. Nae huyo, ndio maana wanawake wanamwita Domo, hiyo yote ni halakati ya kujisifu kama muhusika ni yeye, atakaga na ujinga wake pamoja na umarufu alionao, Hawa wanawake wa bongo wanamdanganya tu, kwamba wamepata mimba zimetoka, ashukuru Zari amemsitiri na hili za kudanganywa mimba zinatoka, lasivyo mambo yangemuendea kombo bila ya kizazi cha Zari, Zari na yeye wanaendana damu zao, ndio maana inamuwia angalau kipata watoto, lakini wanawake wa bongo Kila siku ingekuwa akivuta chake mimba imetoka

    ReplyDelete
  3. Da mtoto mzuri huyu, huyu demu ni mzuri sana sijawahi ona, amewapita hata akina Wema sepetu, Lulu Michael, Agnes masogange, Irene uwoya, na yule mchaga ambaye yupo na Harmonize, yaani amewapita wasanii wote kwa mpigo kwa urembo wake ana urembo wa kipekee sijui Majai alirogwa na Lulu mpaka Majai akamuacha huyu demu sababu huyu demu ni murembo sana kumpita Lulu mara mia nasemea hivyo mimi nikiwa naishi Ulaya na ninajua maana ya urembo, huyu demu akija Ulaya wanaume wazungu watampenda sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uzuri wa mwanamke sio urembo, .............

      Delete
    2. Hata Africa Kuna wanaume sio ulaya tu, uzuri si Hoja Bali tabia,hata hao wa ulaya wanapendi mwanamke asie na tabia nzuri, kwanza uzuri wa sasa upo madukani, huo ni urembo tu, unaofanya mwanamke avutie, na kama ni wembamba ni kawaida, Huyu mnene Huyu mwembamba, na uzuri upo machoni pa mtu mwenyewe kwa mtazamo wake

      Delete
  4. Da huyu demu kaumbika yaani anacho kila kitu, cha kwanza ni sura nzuri saana kabisa, cha pili umbo zuri saana tu, cha tatu ni rangi nzuri saana halafu huwa haringi wala hajidai kuwa yeye ni mrembo kama akina Lulu ambao hata sura hawamfikii hata kidogo huyu demu kwa urembo Wake lakini hao kina Lulu wanaringa mpaka wanapiga mipicha ya nusu uchi. Da huyu demu Mobeto akija huku Ulaya wanaume watamfuata kama kumbi kumbi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad