Diamond: Dalali Alishangaa Watu Wengi Kuulizia Nyumba Niliyonunua SA

Diamond amedai kuwa idadi kubwa ya watu, hususan kutoka Tanzania ilikuwa ikipiga simu kwa wakala aliyekuwa akihusika na mauzo ya nyumba aliyonunua Afrika Kusini kutaka kujua kama ameinunua kweli nyumba hiyo au alipiga changa la macho.

Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, Jumamosi iliyopita, Diamond alisema wengi walikuwa wakiiuliza nyumba hiyo kinafiki
hadi wakala alishangaa imekuwaje! “Baada ya yale maneno maneno, hata yule agent alishangaa ‘hii nyumba mbona sasa hivi inauliziwa’ maake ile wikiendi iliulizwa sana sababu birthday ya Zari ilikuwa Ijumaa so wikiendi kuanzia Jumamosi, Jumapili watu wakawa wanaenda eti kujaribu kutrack ‘vipi nyumba inapatikana.’

Kwahiyo baada ya hivyo wenye nyumba hata wakashangaa ikabidi Zari akawaambia kwamba mpenzi wangu ni celeb na ndio maana alivyopost watu wanaulizia kinafiki,” alieleza. “So baada ya hapo basi ikawa easy wakaitoa kwenye mtandao kabisa, halafu wakaweka kibango kwamba ‘sold out’ wamesahau tu chini kuandika Nasib Juma,” aliongeza Diamond.

Kwa upande mwingine staa huyo amedai kuwa aliinunua nyumba hiyo wa fedha alizozilipa mara moja ambazo ni takriban shilingi milioni 394 pamoja na fedha za transfer zaidi ya milioni 20. Diamond anadai hatua inayofuata ni kwenda kuipamba kwa kumtumia mtu wake wa decor. “Nataka kwanza nikapatengeneze, hapo sasa nataka kufanya ushembenduzi, watu wanafikiri nimefanya, kumbe bado sijafanya sababu vitu kama hivyo lazima uwe proud kwasababu mimi nimekuwa katika mazingira magumu sana kutoka Tandale,” alisisitiza.

“Kwahiyo ile kwangu mimi ni achievement kubwa, kumiliki nyumba South Africa sio kitu kidogo, na ndio maana nataka nikapapambe vizuri nikapitie njonjo haswaa halafu nikiingia South Africa ni mashauzi mengi sana. Of course sometimes you need to do that sababu unafanya kazi kwa bidii.”

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. eti wamesahau pale chini kuandika Nasibu juma sio kwamba wamesahau hawajaandika hivyo sababu wewe si mnunuzi wa hiyo nyumba ndiyo maana hawawezi kuandika jina lako, utadanganya mpaka lini Diamond ujue ukweli mwisho wa siku hujulikana wee danganya tu kuwa umenunua hiyo nyumba endelea tu kudanganya siku ikigundulika kuwa siyo nyumba yako utachekwa tena itakuwa ni aibu ndiyo hapo utajifunza kuwa uongo ni mbaya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ifike wakati kubalini kuwa mungu hutoa utakapojituma na kumuomba,acheni choyo,dogo ndo keshapenya,pigeni kazi nanyi mungu atawafungulia,pia hakikisha nafsi yako pia haina kutu,zingatia hayo niliyoandika Anonymous 5:28

      Delete
    2. acheni wivu mtaugua vidonda vya tumbo bure wakati mambo hayawahusu, nyie kila siku kumkwaza mototo wa watu

      Delete
    3. wewe Anonymous 2016: at 8:33, unamtetea Diamond wakati anadanganya kuwa nyumba ya watu aniita ya kwake, we subiri tu, uongo mwisho wa siku hujulikana,atachekwa uongo ni mbaya

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad