Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa amechambua mwaka mmoja wa uongozi wa Rais John Magufuli tangu aingie madarakani akisema kuna mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha ya wananchi yamezidi kuwa magumu.
Lowassa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 aliungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema hayo jana katika andishi lake kwa vyombo vya habari.
Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kujiuzulu mwaka 2008, amesema katika andishi hilo kwamba, “kile ambacho tulikisema wakati ule kwa nini tunataka mabadiliko, hivi sasa kila mtu anakiona.
“Kwamba pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka, elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa, utumishi wa umma umekuwa kaa la moto.”
Edward Lowassa Anena Mwaka Mmoja wa Rais Magufuli
26
October 26, 2016
Tags
"KUMBUKA KUWA ROME HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA" HATA KAMA WEWE NDIYO UNGESHINDA UCHAGUZI ULIOPITA NA KUWA RAIS WA TANZANIA INGEKUWA HIVYO HIVYO KUHUSU HALI YA WATANZANIA TENA LABDA INGEKUWA HOVYO KUZIDI HII HALI JINSI ILIVYO ACHA KUCHONGANISHA AU KUWACHANGANYA WATANZANIA VICHWA KWA AJILI YA MANUFAA YAKO BINAFSI AU YA CHAMA CHAKO KUMBUKA MANENO MATUPU HAVUNJI MFUPA
ReplyDeleteEnter your comment...lowassa siasa uchwara hazina nafac kwassa ungekuwa wewe ungeuza hadi nchi
ReplyDeleteNi muda mfupi kuanza kumlaamu JPJM kwa kuwa bado anajaribu kuibadilisha TZ kutoka kule mlikoiacha wewe na wenzio enzi hizo ukiwa waziri mkuu.Kama unakubali kuwa yako maendeleo machache ni vyema,kumbe ni swala la kumpa ushirikiano tu ili aendelee kulisongesha gurudumu.Mungu mbariki rais wetu,Mungu ibariki TZ.
ReplyDeleteHAPANA JAMANI.AU NDIO SIFA ZA UPINZANI KUPONDA KILA JAMBO?HIVI WATANZANIA SIJUI TUMELOGWA NA NANI?NI NANI ASIYEONA JUHUDI ZA MUHESHIMIWA JPJM KWA KIPINDI KIFUPI HIKI?UNGEKUWA WEWE MH.LOWASA KWA MWAKA MMOJA HUU SIJUI TUNGEKUWA WAPI,SITAKI KUAMINI KAMA UNGETHUBUTU HATA KUKEMEA AU KUTUMBUA JIPU HATA MOJA,LAKINI YEYE AMETHUBUTU.MUNGU WETU MPE UHAI NA AFYA NJEMA RAIS WETU
ReplyDeleteNi kweli maisha sio magumu?. Ni kweli utumishi si kaa la moto? Ni kweLi Ajira hajawa bomu? Sipend siasa Nataka tutazame kwa ukweli. Nenda huko shuleni ukajionee Kuna nn? Pia huyo mzee edo anabusara kwanza kasema zipo sehemu rais amefanya vzr. Sasa Kuna ubaya gani.
ReplyDeleteSwali ni kwa muda gani?yeye alipokuwa waziri mkuu alifanya nini?
DeleteACHA SIASA UCHWARA.
Mbona ulipokuwa waziri mkuu hukuthubutu kukosoa?kulikuwa hakuna mapungufu?AU?
ReplyDeleteBaba hebu nyamaza kushabikia siasa za akina Mbowe,tunakuheshimu na hatutaki kukutolea maneno yasiofaa.Tatizo la ajira hata wakati wewe ukiwa kiongozi serikali lilikuwepo,mbona hukushauri kutatua kama unaona ni rahisi kwa mwaka mmoja huu tu?na tena wakati ule watoto wenu ndio walikuwa kwenye sekta nyeti bila kujali sifa walizokuwa nazo,mahali kama BOT na kwingineko waliofanya kazi wengi ni majina ya watoto wa vigogo tu,kama sio mashemeji zetu.Mungu ni mwema mnaumbukaje sasa?NA BADO!
ReplyDeleteTumeshtuka!Mnataka mabadiliko wakati nyie wenyewe mmejimilikisha mashamba yasiyoendelezwa na mnakaa nyumba za NHC bila kulipa?Kwanza Muheshiwa rais amesema haya maisha magumu ni ya mpito tu.Mtuacheeeeeeeeeeeeee na jembe letu.
ReplyDeleteMhe, Lowassa naona ni muda mrefu watu hawajakusikia na lo umeonyesha kumbe upo?mbona ujabadilika wewe kwanza? issue hapa usione wananchi tumekaa kimya tunawaangalia wewe na mwenzako kweli mnaweza kuleta mabadilikoau wameamua kuwa na nyinyi kwa sababu za Ukanda na Ukabila?kwa kifupi Dr JPM amefanya mengi kwa muda mfupi ambayo uenda wewe ungechukuwa zaidi ya miaka 20 na mengine usingegusa, hasa bandari na Tra. Mhe, wewe kwa mfano ungeamua kuhamia Dodoma lini? ikiwa ulisema ukishindwa urais unarudi kwenu Mondulikuchunga mifuko lakini umeshindwa. Wewe muache mwanaume afanye kazi sasa mtu aingilie kwa nia ya kuharibu aone.Mhe,kuirejesha mahali pake tanzania iliyoharibiwa maksudi lazima tumwake damu na kufunga mkanda na mwisho wa siku tutafika, nyie endeleeni na kesi mahakamani hakuna kazi nyingine kwani kila kitu tamabarare ila hakuna deal mzee.ALUTA CONTINUA.
ReplyDeleteUkiniambia nitaje list ya watu wanaostahili kuwa marais wa nchi hii au viongozi wa nchi hii tukiacha JPJM,bila kujali vyama vyao na wana uchungu na wananchi huyu simpi hata namba ya 1000.
Delete1.Samia.CCM
2.Majaliwa.CCM
3.Mchemba.CCM
4.Ana Ngwira.ACT
5.Lipumba.CUF
6.Mwita.CHADEMA
7.Makonda.CCM
mmh,kwa leo inatosha nitaendelea.
Yah baada ya miaka 10 ya Magu CCM tunakuja na rekodi nyingine ni siri ila soma USA!!!
DeleteAkajambe mbelee uko
ReplyDeleteHuyu nae VIP, si atulie aone kwanza, kwani uko nyuma yalikuwa nafuu, mxiuu nafuu ya kutoka wapi? Hao wachache waliokuwa mafisadi? Hao ndio ilikuwa nafuu kwao, lakini si kwa mwananchi wa kawaida mxiuu, akajambe mbeleee kule
ReplyDeleteKUBALI TU KINACHOENDELEA BABA,WAFANYAKAZI HEWA,VYETI FAKE,UFISADI TUPA KULEEEEEEEEEEEEEE.
ReplyDeleteSASA HIVI KILA MTU ANAKULA KWA UREFU WA KAMBA YAKE,MLITUNYANYASA SANA NA WATOTO WENU,INATOSHA.ACHA TUISOME NAMBA WOTE.
ReplyDeleteHeee! Hivi huyu 'BABU' yupo jamani....?!?! Hajaenda tu Monduli kuchunga ng'ombe kama alivyomwambia Zuhra Yunus wa BBC kwamba akishindwa ktk uchaguzi atarudi kwao!!! hahaha HAPA-KAZI-TU, hakuna kujenga UKUTA wa 'biscuit'...........Lip Lip Lipumba
ReplyDeleteYeye angeacha mafisadi na wezi wakwepa kodi wamwage pesa za wizi mitaani halafu wasema maisha tambarare,, Haiwezekani na sasa hivi maisha ya kugushi gushi hayana nafasi ndio maana unasikia vilio tu kona zote ohh maisha magumu ohh maisha magumu ulishawahi kusikia kuna serikali inatoa pesa za mgao??? acha hizo bwana tuko vizuri na leo unaona nchi jirani karibu zote wanaomba Magu angekuwa wao alafu wewe unatuambia NINI??? Wewe uwe raisi na LEMA awe Waziri Mkuu na Mbowe makamu wa raisi orrra!!!
ReplyDeleteHahahaha! Lowasa,Lema,Mbowe?si nchi itauzwa?
DeleteDuh! List ya 'wapiga-dili', saa hizi tungekuwa tuna-pumulia mashine......mkate mmoja sh. 20,000 ....ahsante Mungu kwa kutunusuru na hilo janga.....
DeleteHuyo babu wakati yupo serikalini yeye alikuwa busy kuiba pesa na kujigawia viwanja yeye oeke yake leo hii anathubutu kufungua kinywa chake bila ya aibu na kumkosoa Rais kweli nyani haoni kundule
ReplyDeleteWabongo wa sasa hivi ni wajanja na waelewa kisawasawa what's going on siyo kama wale wa enzi hizo kwa hiyo mtu mzima husitake kujiaibusha bure umeishaliibia taifa la Tanzania vya kutosha kwa hiyo kaa point ule mali zako za haramu ulizowaibia watanzania wenzako ambao leo hii unajidai kuwa na uchungu nao ili mradi upewe urais ili iweje au nao unataka kuwauza nini?
ReplyDeleteMdau kula tano. Wabongo wa wazamani sio wa sasa. Asitufanye wajinga. Huyu baba enzi za uongozi wake amepiga dili aswa za kutuibia, sasa anaona mziki mnene, anayapa tapa Huyu fisadi mkubwa sana anatakuleta zake za kujishebedua, sio sasa, mambo hayarudi nyuma Bali yanaenda mbele,
DeleteMtunguo we! Vivyo unaijua siaasa au unajifundisha na Kujaribu siassa Uchwara?
ReplyDeletePoa sie yetu macho na ukianguka tutakupeleka Sibitali kupata huduma ya Kwanza.
Hili Jembe habari nyingine na spidi yake msalie mtume.. Wewe kaa pembeni ushangilie tuu.. Huyu hana Masika wala Kiangazi ndiyo tukaita JPJM ( Jua PasiPo Jua Mvua -Mbele kwa Mbele usije kuwa Majeruhi Edo. Pumzika jiangalie afya yako na Fedeliki na Towe.. Hapa Kazi tu. Mungu amlinde JPM
Mtunguo we! Vivyo unaijua siaasa au unajifundisha na Kujaribu siassa Uchwara?
ReplyDeletePoa sie yetu macho na ukianguka tutakupeleka Sibitali kupata huduma ya Kwanza.
Hili Jembe habari nyingine na spidi yake msalie mtume.. Wewe kaa pembeni ushangilie tuu.. Huyu hana Masika wala Kiangazi ndiyo tukaita JPJM ( Jua PasiPo Jua Mvua -Mbele kwa Mbele usije kuwa Majeruhi Edo. Pumzika jiangalie afya yako na Fedeliki na Towe.. Hapa Kazi tu. Mungu amlinde JPM
Mtunguo we! Hivyo unaijua siaasa au unajifundisha na Kujaribu siassa Uchwara?
ReplyDeletePoa sie yetu macho na ukianguka tutakupeleka Sibitali kupata huduma ya Kwanza.
Hili Jembe habari nyingine na spidi yake msalie mtume.. Wewe kaa pembeni ushangilie tuu.. Huyu hana Masika wala Kiangazi ndiyo tukaita JPJM ( Jua PasiPo Jua Mvua -Mbele kwa Mbele usije kuwa Majeruhi Edo. Pumzika jiangalie afya yako na Fedeliki na Towe.. Hapa Kazi tu. Mungu amlinde JPM