Hatukuomba Kuja Bariadi, Hatuna Uwezo wa Kurudisha Fedha za Mwenge – Madereva

Madereva na wasidizi wa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mbalimbali waolikuwa tayari wameshafika mkoani Simiyu kwaajili ya kusherehekea kilele cha mbio za mwenge, wameeleza kuumizwa na agizo la Rais John Magufuli la kurejesha fedha za kujikimu.

Baadhi wamesema kuwa hawana uwezo wa kuzirejesha fedha hizo kwani hawakuwaomba kufanya safari hizo kwwakuwa ilikuwa sehemu ya kazi zao kwahiyo kiasi cha fedha hizo walizitumia kama walivyokubaliwa na ofisi kuwawezesha na kufika katika eneo hilo.

“Sisi hatukuomba kuja Bariadi kwenye sherehe za mbio za Mwenge wa uhuru, tuliambiwa kuja na tukapewa fedha ambazo tumezitumia kwa mujibu wa mahesabu ya matumizi tuliyoandikiwa kwasababu ilibidi tule na kulala kwenye nyumba za wageni,tutapata wapi hela za kuzirudisha, hapo sisi kosa letu liko wapi,”? alihoji mmoja wa madereva aliliambia gazeti la The Citizen.

“Ili nibidi nilipe chumba kwa siku 7 ambazo nilitarajia kuishi hapa kama nilivyotumwa kwa uhaba wa vyumba,sasa naanzaje kumwambia mmenyewe arudishe fedha yote ili niirejeshe ofisini ?alihoji.

Wiki iliyopita Rais John Magufuli alisitisha safari ya viongozi wa mikoa na wilaya kwenda Simiyu kwenye kilele cha mbio za Mwenge na kuwataka wale waliokwisha chukua posho kuzirejesha.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kinachotaka kuonekana hapa ni kusema kwamba kiendacho kwa mganga hakirudishwi na kwamba pengine Mheshimiwa Rais alichelewa kutoa agizo la kutokwenda Bariadi.
    Rais analenga kuokoa fedha za taifa ingawaje kwa kukawia kidogo, hasa kama ndivyo ilivyo.
    Muhimu ni kuangalia ni fedha ipi ilikuwa haijatumika irejeshwe na ipi ilishatumika iachwe. Wenye nyumba za kulala wageni iwapo walipokea fedha za wateja wao za siku saba na wateja wao hawakulala kwa siku hizo saba basi fedha za siku ambazo hawakulala zirejeshwe.
    Mafuta ya magari ambayo yalishanunuliwa itakuwa vigumu kurejesha fedha zake.

    ReplyDelete
  2. Hii ni stori ya mwandishi anataka tumuelewe vibaya muheshimiwa raisi kama kawaida inavyojulikana aliyefika hadaiwi kurudisha pesa kwa sababu lazima ajikimu na maisha na hilo ni jukumu lipo kwa mabosi wao kwa vile wanajua pesa zilitumika vipi na sio mwandishi na kama madereva na wasaidizi walikuwa wajaondoka sehemu zao kwenda kulikokusudiwa inabidi kuzirudisha pesa kwa sababu safari imevunjika ila hapa mwandishi anaandika hisia zake na sio madereva au ndo chendacho kwa mganga hakirudi bora angetufahamishe hivyo mwandishi sio kutetea utapeli kwa njia ya udanganyifu

    ReplyDelete
  3. jambo ni dogo tu. Agizo linaeleweka.kama ulicgukua Mil lumi na umetumia laki. chukua tena laki kukurudisha lituoni kwako. Tupe risiti halali za laki mbili na balance ya mil tisa na laki nane ..mbona inaeleqeka kiurahisi au kuma ugumu wa kukumlisha na kutoa...Hapa kazi tu

    ReplyDelete
  4. kwani hajuwa toka mwanzo
    tatizo Msoga umetuletea balaaa huyu mkuu mropokaji hataki ushauri yeye anajuwa kila kitu Mnyatunuzu haachi jadi
    anaropoka na kukurupuka yeye na kina makonda wake
    fyuuuuuuuu
    sifa haijii hivi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna cha kukurupuka wala nini nyau wewe mlizoea vya kunyonga wewe ndo fyuuuuuuuuuuuuuu usitukane kabila kwa jaziba ya ushabiki

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad