Jamhuri Kiwelu Julio baada ya mechi hiyo aliongea na waandishi wa habari na kusema kuwa saivi atakuwa anaenda kuangalia mpira uwanjani ila hawezi tena kuwa kocha wa mpira Tanzania.
“Kuanzia leo na kuendelea, sitaki tena mpira. Najiuzulu mpira moja kwa moja sitaki kwasababu mpira wa Tanzania unachezwa kwa siasa sana. Mpira unachezwa kwa ajili ya kufurahisha watu hata wasiokuwa na uwezo waonekane wanajua, hiki kitu kinaumiza sana”, amesema Julio baada ya mchezo kati ya Mbeya City vs Mwadui uliomalizika kwa vijana wa Julio kulala kwa bao 1-0 ugenini.
“Nimeshafundisha mpira Qatar, Yemen na Dubai lakini sijawahi kufeli lakini kuna kundi la watu wanajua huyu ukimfanyia hivi unamharibia ni kuharibu mpira wetu ndio maana vilabu vyetu vikienda kwenye mashindano ya kimataifa havifanyi vizuri.”
“Kwahiyo kuanzia sasahivi natangaza sitaki kuwa kocha wa mpira wa Tanzania tena labda nikipenda niwe naenda kuangalia mpira lakini kinyume cha hapo sitaki mpira kwasababu tunakoelekea siko. Kuna watu watasikitika kutoka kwangu kwenye mpira lakini kwa kipindi hiki bora nipumzike nifanye kazi nyingine kwanza, mawashuru watanzania wote waliokuwa karibu na Julio.”