JE, ni Maadili Baba Kumnunulia Bintiye ' Pedi ' na Kujua Kuwa Yupo Mwezini?

Siku hizi nimekuwa nikiwaona baadhi ya akina Baba ambao binafsi nawaita wa ' hovyo hovyo ' wakija na Mabinti zao tena wakubwa tu Madukani na hasa katika Supermarkets mbalimbali na kuwanunulia ' Pedi ' tena kuna wakati unakuta ' Li Dingi ' hilo hilo bila hata chembe ya aibu linamchangulia ' Bintiye ' aina ya ' taulo ' za kutumia.

Kama hii haitoshi hivi punde tu wakati na Mimi nikipanda Mti wangu nilioubatiza ' Le Mathematicien GENTAMYCINE ' niliweza kumsikia ' mubashara ' kabisa Baba mmoja akiongea na Simu na Mtu mwingine kuwa akimaliza tu kupanda Mti anataka kupitia dukani kumnunulia ' Bintiye ' taulo za Kike ' Pedi ' kwani alipotoka tu nyumbani kwake asubuhi hii alivyomuona tu alihisi kuwa ameanza safari yake ya kwenda ' Moon '.

Najua humu kuna akina Mama zetu na Wazee wenye MAADILI kabisa hivi haya mambo ya ' hovyo hovyo ' wayafanyayo Wazazi wa siku hizi hasa wa Kiume kwa Mabinti zao hususan kuwanunulia ' Pedi ' na kujua kuwa wapo ' Moon ' wamerithi kwenu nikimaanisha kuwa na nyie huko nyuma mlikuwa mkifanyiwa hivi au ni ' Uzungu ' tu umetuharibu na tunakosa maadili na kujua mipaka ya Baba juu ya Binti yake ambaye ni mkubwa na ameshavunja Ungo?

Badilikeni Wanaume wenzangu na akina Baba na jifunzeni kujua mipaka yenu hasa kwa Mabinti zenu.

Asubuhi na Jumamosi njema nyote.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kila kitu lawama "UZUNGU" mambo mengine mnawapakazia hawa viumbe bure kumbe ni ulimbukeni wetu wenyewe kwa kufanya au kufikiria kuwa hivi tufanyavyo ni kama wazungu yaani babkubwa kumve hovyooooooooo!!!upuuuziii pesa mwanadamu akiwa nayo hufanya mambo ya ajabu ajabu wakati mwingine

    ReplyDelete
  2. Acheni ushamba yalikuwa zamani
    Hedhi si ugonjwa kwa wanawake
    Hata mama namnunulia pedi ni ndiyo walivyoumbwa na mungu

    ReplyDelete
  3. ni kawaida sana. ulipoanza kuandika nilidhani kun ajambo la aibu kumbe ni hilo? ni upendo tu japo hutegemea na utamaduni wa kila familia, sio dhambi pia kwani ni familia yake aliyoizaa mwenyewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ila ndugu mipaka lazima iwepo ili kulinda heshima na thamani ya mtu!! Hii ndiyo matokeo yake watu wanatamaniana kisa kujua mambo ya sirini ya mtoto/mama yake!! tuache upumbavu!! hata kama ni baba au kijana wako wa kiume bado ni mwanaume! na mwanaume lazima awe na mipaka kwa mwanamke ambae anatakiwa kumuheshimu.Period

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad