Jicho la 3: Maajabu ya goli la Tambwe, na jinsi waamuzi walivyoibeba Simba muda mwafaka katika goli la Kichuya

Na Baraka Mbolembole

‘NI Ujinga’ kufikiria unaweza kupata matokeo mazuri wakati unachofanya ni kile kile kila msimu na kinakuletea matokeo mabaya.

Timu gani ilibebwa katika Yanga 1-1 Simba? Ni Yanga? Kwa vile labda walifunga goli uliloliona ni ‘tata’? Ama ni Simba ambao walisawazisha dakika 3 kabla ya kumalizika kwa mchezo kwa mpira wa kona ya moja kwa moja? Ama, labda ni uwezo mdogo wa mwamuzi Martin Saanya na wasaidizi wake?

‘MPE SIFA MBAYA TAMBWE, NAYE ATAKUNG’ATA SEHEMU INAYOUMIZA’

Mshambulizi huyu wa timu ya Taifa ya Burundi anahitaji kufunga walau goli moja tu katika ‘Dar es Salaam-Pacha’ ili kusimama pekee kama mfungaji wa muda wote wa game za Yanga vs Simba.

Aliifunga Yanga mara mbili wakati alipokuwa mchezaji wa Simba katika game ya Nani Mtani Jembe, Desemba, 2013 katika ushindi wa Simba 3-1 Yanga.

Mtaalam huyo wa magoli ya kichwa akaifunga Simba mara mbili katika game mbili za VPL akiwa na kikosi cha Yanga msimu uliopita (Yanga 2-0 Simba, Oktoba, 2015, Simba 0-2 Yanga, Februari, 2016) na goli lake la Tatu vs Simba alifunga katika game ya Jumamosi iliyopita.

Kiujumla, Tambwe ameshafunga magoli matano katika mipambano 7 ya mahasimu hao wa kandanda la Tanzania.

Ni rekodi ya aina yake ambayo sasa imemfanya kusimama na Watanzania, Emmanuel Gabriel na Jerson Tegete ambao pia wamefunga mara tano katika ‘PACHA’ hiyo yenye kuvutia wapenzi wengi wa kandanda Tanzania na Afrika Mashariki.

Wakati, Gabriel alifunga magoli yote vs Yanga na Tegege akifanya hivyo akiwa mchezaji wa Yanga vs Simba, Tambwe amefunga kila upande na kuna washambuliaji wengi waliopita katika timu zote hizo lakini tangu mwaka 1935 ilipozaliwa rasmi Yanga kisha, 1936 ilipozaliwa Simba hakuna aliyeweza kufanya kama alichofanya Tambwe katika pambano hilo.

Tambwe ni kiboko na goli lake la tano amefunga na kupelekea matukio mengi yatakayobaki. Kwa furaha na majonzi.

Huyu ndiye ‘Mr.Hat-trick’ ambaye amejiwekea rekodi ya peke yake ya kufunga katika michezo mitatu mfululizo ya Yanga vs Simba. Goli lake lilikuwa ‘bab-kubwa’ na hata wakufunzi wa Simba watakuwa wamejua uwezo alisi wa beki wao kijana, Novatus Lufunga.

Beki gani makini anaweza kujipanga katika mtindo ule wa Lufunga? Yaani, anamuwekaje mshambuliaji ndani ya eneo la hatari na wewe beki unakaa nje? Nilisema kabla ya mechi kwamba mipira ya juu ni tatizo kubwa katika safu ya ulinzi wa kati upande wa Simba na Mbuyu Twite akathibitisha hilo kwa pasi moja tu timilifu.

Tambwe utamchukia wewe, lakini sifa yake itapendwa na wapenzi wengi wa kandanda nchini. Halafu, hivi ‘mkuki kwa nguruwe, Eeh?’ Tambwe si wa kwanza, Mzee wa Kiminyio, 2001 Fainali Tusker Cup, Simba 4-1.

Pasi ile ndefu ya juu ilipigwa kwa malengo ya kufika kwa Tambwe na Mrundi huyo akamuweka nje ya eneo la hatari, Lufunga na kuuthibiti mpira wa juu mbele ya mtu mrefu zaidi yake. Bonge moja la mbinu, dakika ya 24 akaleta tofauti ya timu bora kimbinu na timu isiyo na uzoefu.

Ni goli safi kabisa, kwani mfungaji alipogeukia ndani ya box huku Lufunga akifuata nyuma yake akaongeza utulivu tu huku akifahamu jaribio lolote la kuzuiliwa na mlinzi huyo wa Simba lingezaa mkwaju wa penalti na red card juu.

Akamchambua tu golikipa, Vicent Anghban. Hakuna goli la mkono katika soka. Maajabu yakaanza, mashabiki wa Simba wakaanza kung’oa viti majukwaani. Wakaanza kuimba, ‘refa, refa, refaaaa’ wakaimba weee.

Walikuwa wanashangaza sana. Goli safi, kadi nyekundu ni halali. Sikuona tatizo la mwamuzi wa kati, Martin Saanya hadi kufikia dakika ya 27 alipomuondoa uwanjani kwa kadi nyekundu nahodha wa Simba, Jonas Mkude.

JUUKO NDIYE CAPTEIN SI MKUDE

Ukweli ni kwamba nimeona jinsi mechi ilivyochezwa. Simba licha ya kuwa pungufu kwa zaidi ya dakika 65 walicheza kwa pamoja na kasi, mpira wa kufurahisha wakati fulani kiu ya kusaka magoli uwanjani. Hali hiyo ilionekana zaidi mara baada ya wachezaji mlinzi wa kati, Juuko Murishid na kiungo wa kati, Mohamed Ibrahim walipoingia uwanjani.

Moja ya mbinu iliyowasaidia sana ni kumtumia Shiza Kichuya ambaye alihakikisha kila anapokuwa na mpira anafuatwa na wachezaji wawili hadi watatu. Juuko aliwahamasisha wachezaji wenzake na kuipeleka timu kwa kasi katika upande wa Yanga.

Simba haikuwa na kiongozi yeyote uwanjani hadi alipoingia Juuko. Mkude anapaswa kulaumiwa kwa kukubali kadi isiyo na faida kwani tayari mwamuzi alishanyoosha mkono wake kuelekea kati mwa uwanja akimaanisha ni goli. Simlaumu sana Mkude ila akiwa na kitambaa cha unahodha ameonesha yeye si kiongozi mzuri.

MARTIN SAANYA

Septemba 28, 2013 mwamuzi huyu wa kati alichezesha game ya ligi kuu Tanzania Bara kati ya Yanga na Coastal Union ya Tanga katika uwanja wa Taifa. Na kitendo cha kuipata kiki ya pemati timu ya Coastal kilimfanya akafungiwa mwaka mmoja na aliyekuwa msaidizi wake Jesse Onesmo.

Mwamuzi huyo mwenyeji wa mkoani Morogoro amekumbwa na lawama nyingi mara baada ya kumalizika kwa game ya Yanga v Simba siku ya Jumamosi. Analaumiwa kwa kukataa mpira ambao ulipigwa na Ibrahim Ajib na kuingia golini kwa Yanga, na akakubali goli la Tambwe ambalo wengi wanasema aliushika mpira ule kabla ya kufunga.

Ajib hakufunga kwa kuwa mshika kibendera alikuwa ‘shabiki wa Yanga’. Mwamuzi wa pembeni ndiye wa kulaumiwa pale na si Saanya. Mwamuzi huyo alijitahidi sana kuchezesha mechi ile lakini waamuzi wa pembeni wakaharibu mechi.

Walikuwa na mapenzi binafsi-yule aliyekataa mpira ulioenda nyavu na huyu ambaye alikubali Kichuya apige kona wakati mpira ulipaswa kuwa wa kurushwa.

MPIRA WA KONA YA KICHUYA ULIKUWA NI WAKURUSHWA

Ally Mustapha ‘Barthez’ anafungwa magoli ya kizembe katika game nyingi vs Simba na mara nyingi katika michezo ya karibuni ya mahasimu hao, Yanga huangushwa na magolikipa. Goli gani lile la kufungwa kwa kipa mzoefu kama Mustapha?

Alifungwa magoli marahisi na Gilbert Kaze na Joseph Owino katika sare ya 3-3 Oktoba, 2013 na akafungwa goli lingine la kuudhi na Emmanuel Okwi katika kichapo cha 1-0 ambacho Yanga walikipata, Machi, 2015 sasa amefungwa goli la kona ya moja kwa moja.

Hakuwapanga walinzi wake ambao wangeweza kumsaidia kuzuia mpira kuingia golini. Ndiyo, mpira ule hakupaswa kupigwa kona lakini mshika kibendera na pengine Saanya mwenyewe walikubali mpira wa kurushwa kuwa kona.

Rejea kuitazama vizuri video kabla ya Kichuya kuupiga ule mpira. Mwamuzi wa pembeni mara baada ya mpira kutoka uwanjani anaonekana akiashiria ni mpira wa kurushwa lakini Ball boy aliuweka mpira katika eneo la kupigia kona na kumwacha Kichuya aupige mpira ambao sekunde chache nyuma anaonekana akionyesha ni mpira uliopaswa kurushwa.

Kama ni upendeleo, Yanga walipendelewa kwa goli halali lililokataliwa na Simba nao walibebwa na kusaidiwa na waamuzi hao kupata goli la kusawazisha dakika 3 kabla ya kumalizika kwa mchezo.

Shafii Dauda
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inasemekana siasa imeingia kwenye football,na kwamba habari za mitaani ni kwamba ubingwa utakuwa kwa zamu,kwa maana hiyo kunatimu inaandaliwa kwa mwaka huu...???????kwa nini tusiamini sasa?

    ReplyDelete
  2. Acheni ushabiki usio kuwa na maana hamjengi Bali mnabomoa goli la kona liwe offiside tatizo usimba na uyanga umewakaa sana soka latanzania ndivolilivo kama hawajabebwa simba yanga lazima hamnampira tz nikudanganyana

    ReplyDelete
  3. Acheni ushabiki usio kuwa na maana hamjengi Bali mnabomoa goli la kona liwe offiside tatizo usimba na uyanga umewakaa sana soka latanzania ndivolilivo kama hawajabebwa simba yanga lazima hamnampira tz nikudanganyana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umekurupuka!Goli linalozungumziwa ni liwe wanalolalamikia simba la Ajibu na muamuzi kukataa.

      Delete
  4. Replies
    1. Ndio akili za kuvunja viti hizo.Sasa hapo umefaidika nini zaidi ya kuigharimu club kulipa?

      Delete
  5. shafi wewe tunajua ni yanga, nilidhani kama mchambuzi makini ungeeleza udhaifu wa timu zote na waamuzi wote lakini badala yake unaoonyesha uyanga. Nilikuwa nakuamini sana lakini kwa kuwa bias umeonyesha udhaifu wako. Ndo maana yanga walipoomba kutumia uwanja wa Amani Zanzibar ukasoma utaratibu/kanuni mwenyewe kuwa uwana lzima uwe bara, lakini bado kwa uyanga ulionao ukasema yanga kucheza Amani stadium ni sawa. wewe ni mmoja wa wanaowasema TFF kuwa wanavunja taratibu kisha wewe unasema ni halali yanga kuchezea mechi zake za ligi zanzibar, utaratibu/kanuni ulisoma mwenyewe nikiwa nasikiliza kipindi cha sports kinachoanza saa tatu usiku.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad