Mahakama Yaitupilia Mbali Kesi Ya Mbowe Hotels Dhidi Ya Shirika La Nyumba La Taifa (NHC ) Maha

Mahakama kuu kitengo cha Ardhi imetupilia mbali kesi ya maombi ya kurejea katika jengo iliyokuwa ofisi ya Tanzania Daima pamoja na ukumbi wa bilcanas.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, Sivangilwa Mwangezi ambaye amesema kuwa taratibu zote zilifuatwa kuondoa vitu katika jengo hilo.

Amesema katika hukumu hiyo hakuna mtu aliyevunjiwa haki yake ya msingi kutokana na kufuatwa kwa Sheria dhidi ya madai ya Shirika la Nyumba NHC, kwa Mbowe HotelS.

Wakili wa upande wa NHC, Aliko Mwamnenge amesema kutokana na hukumu hiyo Mbowe hotelS wanadaiwa sh. Bilioni 1.7 na NHC.Amesema vitu haviwezi kurudishwa mpaka pale mlalamikiwa atakapolipa deni lake kwa NHC.

Nae Wakili upande Mbowe Hotel, John Malya amesema wamepokea hukumu na kuomba nakala ili kuweza kuifanyia kazi.Amesema kuwa nakala wakiipata wanaweza kuamua katika kukata rufaa.

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Protea si ulipe. Deni baya. Utapoteza vingi. Ukilipa utasaidia maendeleo ya NHC huko Makao Makuu Dodoma. Ujanja Ujanja na Haki za Serikali (Watu+ Wananchi akiwemo J Malya hatuutaki. deni limethibiti ni wajibu wako kujiwajibisha kwa Kulipa au utalivutia kwenye siasa... Joni msaidie kumuelewesha asiye elewa au hataki kuelewa? Hapa ni Uaminifu na Uzalendo. Lipa ndugu yangu uondoe Fedheha inayo kuandama.. TRA wako njiani huko plotea. Hapa Kazi Tu.

    ReplyDelete
  2. Mallya unajua kabisa sheria,ni wazi Mbowe anatakiwa kulipa,Ila kwa kuwa mmeweka U-siasa ndani ya hili unajifanya kutetea,ni aibu sana.Mh.Mbowe lipa deni,ni hela za wananchi sio za Mchechu wala Magufuli.

    ReplyDelete
  3. Mallya ondoa kabisa kichwani mwako kutetea kwa kutumia vifungu fulani ili tu Mbowe ashinde,uliapa kwa ajili ya wananchi wote wa Taifa la TZ,basi fanya kwa ajili ya Taifa la TZ.TANZANIA BILA RUSHWA INAWEZEKANA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad