Jeshi la majini la Marekani na lile la Korea Kusini, kwa pamoja yanasema kuwa, jaribio jingine la roketi ya Korea Kaskazini limeshindwa.
Wakorea Kusini wanasema kuwa, lililipuka mara tu baada ya kurushwa.
Kamanda mkuu wa jeshi la majini la Marekani Gary Ross, anasema kwamba uzinduzi huo uligunduliwa hapo jana Jumamosi karibu na mji wa Kusong.
Roketi hiyo inaaminika kuwa aina ya Musudan na yenye masafa marefu, na inayokisiwa kulipua umbali wa kilomita elfu tatu.
Korea Kaskazini haijasema lolote.