Matani ya Stan Bakora Yamtoa Povu Barakah The Prince

Mchekeshaji Stan Bokora baada ya kufanya cover ya wimbo ‘Nisamehe’ wa Barakah Da Prince kumezuka mtafaruku baina ya wawili hao.

Barakah The Prince amedai hajapenda jinsi Stan Bakora alivyomwigiza katika video hiyo.

Muda mchache baada ya video hiyo kutoka, Baraka The Prince aliandika: Matani ni mazuri ila yakizidi yanaweza kuleta matatizo… heshima ichukue nafasi yake tafadhali mzee utani huu sijaupenda iwe mwanzo na mwisho tafadhali.

Kwa upande wa Stan Bakora alisema kila video ambayo anafanya cover ni lazima azungumze kwanza na mwenye kazi na kukubaliana naye.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Utani wenye ukweli ndani yake,Halafu kwa nini Baraka kachukia na kutokwa na povu?ina maana hajivunii weusi wake?kwani weusi ni ugonjwa?

    ReplyDelete
  2. Pale unaposikia neno"UKWELI UNAUMA"
    Jamaa ni mweusi kweli,na wala sio mbaya kwamba labda kafanaishwa na mwizi,malaya nk,lakini ajabu imemuuma na kutoa povu.

    ReplyDelete
  3. Baraka usikasirike kwani weusi wako ni mzuri ni weusi wa bright, sio kama akina Rich mavoko hawapendi weusi wao mpaka wamejichubua na sio Rich Mavoko tu wako wengi wasanii waliojichubua, lakini wewe umebakia na rangi yako nzuri na inakupendeza sana wala usiibadilishe kama wasanii wengine

    ReplyDelete
  4. Watu tumeumbwa tofauti jamani, wengine hawapendi utani. Pole Barakah take easy.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad