Miaka kadhaa iliyopita, kwa mara ya kwanza Tanzania ilipata mwakilishi kwenye ligi bora ya kikapu duniani; NBA kupitia Hasheem Thabeet. Wapenda michezo na maendeleo kwa ujumla walifurahia uwakilishi huo kwa kile kilichoonekana kutafungua milango kwa wengine. Na kweli, kuingia kwa Hasheem NBA kuliongeza hamasa ya Watanzania kutaka ku-break to NBA Gates.
Ni bahati mbaya Hasheem hakufanya vizuri sana NBA na baada ya miaka michache akajikuta anapelekwa D-League!
Kwa sasa Hasheem ni kama amesahaulika lakini ifahamike tu hajalala! Kwa miaka takribani miwili sasa amekuwa aki-fight kurudi NBA. Rekodi zake za D-League msimu uliopita zilikuwa mzuri na zilitia matumaini kwamba huenda angerudi NBA. Hata hivyo bahati haikuwa upande wake.
Wakati namfuatilia mwaka jana nilipata hofu kwamba kukosa kwake kurudi NBA (mwenyewe alitarajia angerudi) kungemfanya awe disappointed kama ilivyo kwa Watanzania wengi. Hata hivyo, Hasheem ni kama aliongeza struggle za kutaka kurejea NBA ingawaje alikuwa na fursa ya kwenda kucheza ligi zingine nje ya US! Hakutaka… bila shaka anachotaka yeye ni kurudi NBA; period!
Katika kuhakikisha anafanikiwa katika hilo, Hasheem akajiunga na coaching ya Frank Matrisciano na Milt Newton. Hawa jamaa wawili si watu wa mchezo mchezo linapokuja suala la individual training. Lakini kubwa zaidi Hasheem anaonekana kujitambua zaidi na kuonesha ni nini hasa anataka.
Rumors zinazoendelea ni kwamba, timu kubwa tatu za NBA zilituma watu wake kumwangalia for workout kwenye training camp ya Hasheem. Haya yametokea miezi sita tu tangu Hasheem aanze kujifua kwa dozi za kila siku za Matrisciano’s program.
Mtu wa mwanzo kutoa taarifa hizo ni Alex Kennedy kupitia mtandao wa Twitter. Alex ni Managing Editor wa Basketball Insiders.
Kwa mujibu wa rumors hizo, timu ambazo zilijitokeza mwezi uliopita ni LA Leakers, Washington Wizards na New York Knicks.
Waswahili wanasema Kufa Kufaana! Wakati Hasheem alifanyiwa workout na Wizards katika mazingira ya kawaida tu (labda ya kutaka kuimarisha safu yao ya ulinzi) lakini hivi sasa beki tegemeo wa Wizards, Ian Mahinmi atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki 4 hadi 6 kutokana na kuwa majeruhi!!!
Kwa upande mwingine, wakati Knicks na Wizards walipeleka watu wao kwenye kambi ya mazoezi ya Hasheem, LA Leakers walienda mbali zaidi kwa kumpeleka Hasheem kwenye facility yao (ya Lakers) kwa siku mbili for free agent workout.
Trainers wa Hasheem, Frank Matrisciano na Milt Newton wanaamini Hasheem anaweza kurudi NBA! Tatizo ambalo analiona Frank ni NBA Community kuwa na perception ya Old Hasheem wakati Frank, kwa kuangalia improvement ya Hasheem; yeye kama Trainer anamuona Hasheem wa sasa ni tofauti sana na Old Hasheem inayesemekana ni mvivu na mtu asiyependa kujituma.
Ni matumani yangu kadri atakavyoendelea kupata workout ndipo chance ya kurudi NBA inaongezeka. Na bila shaka wapenda michezo na burudani watamuombea our only boy ili aweze kurudi NBA. Nothing impossible under the sun. Hata hivyo, Waswahili husema, Kisicho Riziki Hakiliki... NBA ikigoma si vibaya kuangalia ligi zingine duniani kama vile Euroleague. Umri unaenda, na in fact, muda si mrefu atakuwa beyond the expiry date. Katika hali kama hiyo mtu anatakiwa kuangalia zaidi maisha kuliko career. Hata ligi ya Uchina nayo si haba!