Mkurugenzi Amgomea Waziri Mkuu

AGIZO la Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, kuwataka watendaji wa Serikali kutoa taarifa katika vyombo vya habari juu ya mipango ya maendeleo inayofanywa na serikali, limepuuzwa na Godwin Kunambi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, anaandika Dany Tibason.

Leo baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi uliofanyika ili kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere, muasisi wa Taifa la Tanzania, Kunambi amekataa kuzungumzia lolote juu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu la kuondoa nyumba za tope katikati ya Mji wa Dodoma.
“Siwezi kuongea jambo lolote kwa sasa ninawaachia Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa waongee. Bora ningekuwa nazungumza na radio au TV lakini katika gazeti siwezi kuzungumza chochote, niache tu,” amesema Kunambi alipozungumza na mwandishi wa MwanaHALISI online.

Pamoja na mwandishi kumkumbusha kuwa Mkurugenzi ndiye mtendaji mkuu wa manispaa hivyo ni vyema akatoa ufafanuzi juu ya hatua gani ambazo manispaa yake imezichukua mpaka sasa ili kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kuondoa nyumba za tope na kuboresha miundombinu lakini Kunambi aligoma.

Hivi karibuni baada ya kuanza utekelezaji wa kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi, Waziri Mkuu Majaliwa alijitambulisha kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma na kuwaagiza wakuu wa Idara mbalimbali pamoja na watendaji wa serikali kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa vyombo vya habari.

“Toeni taarifa za utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya serikali katika vyombo vya habari bila kukibagua chombo chochote,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Kitendo cha Kunambi kukataa kuzungumzia mipango ya maendeleo hususani utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu la kuondoa nyumba za tope katikati ya mji ni kupuuza agizo lake la awali la kutaka taarifa muhimu za mipango ya maendeleo zitolewa katika vyombo vya habari bila kuvibagua vyombo hivyo.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwana Halisi, Huu ni udaku na upotoshaji wa Hali ya Juu. Kichwa cha habari ni cha kiuchonganishi na chukivu. Kunambi hakuwa na Nia hii ulivyo ileta kwetu. Nikijaribu kusoma na kutaka kuelewa inadhihirisha aliye muhoji hakuwa na uelewa au hawakuelewana na baina yao ilikuwepo ubishi. Na akaamua kutuletea hivi ili aweze kutia dosari na kutokuelewa baina ya mtendaji na utendaji wake na wenzake. Agizo la Mh Kassimu linaeleweka na yeye kwa hivi sasa ni Mkazi wa hapa kwetu Dodoma na sidhani kama itakuwa ni busara kwenu kuanza kuleta chokochoko baina yetu. Na watendaji wetu wa ngazi za JUU. Kuweni ni Wazalendo katika uletaji habari na mantiki kusudiwa.. Tujenge upendo na Uelewa wakati wote na Elimu Elimu na Busara ni Muhimu... Karibu Mh Majaliwa na Agizo na Maagizo yako tutayatekeleza bila Kusita na kwa Ufanisi wa hali ya Juu. Hapa Kazi Tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, Hawa waandishi wetu ni Bomu. inafikia kama ilivyoondikwa hapo juu." Pamoja na Mwandishi KUMKUMBUSHA kuwa MKURUGENZI NDIYE MTENDAJI MKUU" Hapo tu ikutoshe kumjua huyu muandishi anayo Ajenda iliyojificha na kuweza Kubainisha kuwa Japo Kunambi kashika Wadhifa lakini hajui kazi au si mtendaji au Hajielewei... Inasikitisha kuwa na waandishi CHOCHEZI katika nchi yetu... INASIKITISHA TENA SANA... KUNAMBI ITABIDI AOMBWE LAZI. AU BODI YA WAANDISHI IMKANYE MWANDISHI

      Delete
  2. Mwana Halisi, Huu ni udaku na upotoshaji wa Hali ya Juu. Kichwa cha habari ni cha kiuchonganishi na chukivu. Kunambi hakuwa na Nia hii ulivyo ileta kwetu. Nikijaribu kusoma na kutaka kuelewa inadhihirisha aliye muhoji hakuwa na uelewa au hawakuelewana na baina yao ilikuwepo ubishi. Na akaamua kutuletea hivi ili aweze kutia dosari na kutokuelewa baina ya mtendaji na utendaji wake na wenzake. Agizo la Mh Kassimu linaeleweka na yeye kwa hivi sasa ni Mkazi wa hapa kwetu Dodoma na sidhani kama itakuwa ni busara kwenu kuanza kuleta chokochoko baina yetu. Na watendaji wetu wa ngazi za JUU. Kuweni ni Wazalendo katika uletaji habari na mantiki kusudiwa.. Tujenge upendo na Uelewa wakati wote na Elimu Elimu na Busara ni Muhimu... Karibu Mh Majaliwa na Agizo na Maagizo yako tutayatekeleza bila Kusita na kwa Ufanisi wa hali ya Juu. Hapa Kazi Tu.. Muwalamsaje Kukaya WWoose.

    ReplyDelete
  3. Mnalazimisha habari? Mbona sasa sisi wenye uelewa tunawaona ninyi MWANAHALISI kuwa mko kiuchonganishi na kiupotoshaji tu. TOENI UDAKU wenu hapa.

    ReplyDelete
  4. kama habari zinalerwa kwa mtindo huu. kuna haja ya kurudi chuoni.

    ReplyDelete
  5. Mkurugenzi amgomea Waziri Mkuu. Kivipi?? Kichwa cha habari hakiendani na Maudhui

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad