Model Maarufu wa Bongo Alitosa Kutokea Kwenye Video ya Salome, Alitaka Pesa Nyingi...Diamond


Kuna model maarufu wa Bongo aliyetosa kuonekana kwenye video ya wimbo wa Diamond ‘Salome.’

Model huyo anadaiwa kutaka alipwe fedha nyingi ambazo zilikuwa nje ya bajeti ya staa huyo.

“Bajeti yangu haikuweza kumuafford, na siwezi kufanya kitu kimashauzi wakati bajeti yangu ndogo,” Diamond alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times.


Diamond anasema alichokikosa model huyo baada ya kukataa kufanya video hiyo si fedha tu, bali exposure ambayo angeipata baada ya hapo.

“Si uchawi, sio uongo, sio ushirikina, unavyofanya video na mimi unakuwa mkubwa na inakuongezea dau,” alisisitiza kwa kuongeza kuwa watu kibao humuomba waonekane kwenye video zake bure lakini hukataa kwakuwa ni lazima awalipe.

Diamond amedai hiyo ndio sababu hatokuja kulitaja jina lake kwakuwa atampa kiki na atakuwa mkubwa.

“Nilimuambia, angalia angle zote mbili, angalia kwamba nakulipa kiasi lakini kushiriki kwako kwenye hii video itakuongezea ukubwa zaidi, itakupa biashara nyingi.”

Alitoa mfano kuwa show nyingi za MTV alizowahi kutumbuiza alifanya bure kwasababu alizitumia kukuza jina lake. Anasema wakati mwingine hadi dancers huwasafirisha kwa gharama zake mwenyewe.

“Lakini najua show ninayoifanya pale ikitoka itanipa hela nyingi baadaye. Niliheshimu alichokisema ndio maana sikumind, nilisema naheshimu sababu umejitambua na umeona thamani yako ni nini, lakini bahati mbaya sisi bajeti yetu haikufika huko.”

Angalia Video hapa:

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wemaaaa huyooo....si usemee tu wema alitaka 75m...ili awe salome...

    ReplyDelete
  2. eeehhh... Kweli ni mtoto wetu Wema... sikitu mara nyingine lazima umsaidie dada yako wema manake hata ukimpa hela ya mawese ni poa tu. Si mtoto wa nyumbani hata maza anammindi. na wewe uwe unajipanga na bajeti poa... mtu unajua Idriss kambania kukomboa Range.. sema ungempa kiki si umtaje tu aipate kiki na siyo skando.. Barida Nasibu

    ReplyDelete
  3. Alikuwa ni Jokate.. Manake nilisikia fununu huko machimbo! Mbona umenfanyia Roho mbaya dau lenyewe alitaka milioni na laki mbili tu. Wewe ukampa laki tano ukamwambia nguo zote akimaliza shooting zitakuwa zake.. Si ungemuongezea Basi.

    ReplyDelete
  4. Sasa jamani Saida Karoli ulimpa chake?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad