Mtoa Macho Buguruni Akamatwa na Polisi

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro amesema jeshi hilo limemkamata mtuhumiwa ‘Scopion’ aliyehusika katika matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha eneo la Buguruni jijini humo.

Sirro alitoa kauli hiyo jana Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kujadili usalama katika eneo hilo ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Alisema mtuhumiwa huyo anayejulikana kwa jina maarufu kama Scopion alikamatwa baada ya polisi kupewa taarifa za matukio ambayo ameyafanya ikiwemo la kumchoma kisu, kumtoa macho na kumsababishia upofu, Said Ally.

"Nimesikia wananchi wanalalamika hapa kuwa tumeshindwa kumkamata Scopion, ni nani kwa Jeshi la Polisi asikamatwe, tayari tumemkamata na sheria itachukua mkondo wake, hakuna mtu anayeweza kushindana na jeshi," alisema.

Aidha Sirro alisema baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo na kuhojiwa aliutaja mtandao wake wote na tayari wameukamata, hivyo amewataka wakazi wa eneo hilo kutokuwa na hofu kwani mtuhumiwa huyo hayupo tena katika eneo hilo.

"Najua suala hili bado lipo mahakamani hatuwezi kulizungumzia sana, bahati nzuri alipokamatwa alieleza aliyoeleza na tukafanikiwa kuukamata mtandao wote, hivyo hakuna haja ya kuwa na uwoga eneo hili lipo salama," alisema.

Kabla ya kauli hiyo ya Sirro, wananchi wamelalamikia askari wa eneo hilo ambao walishindwa kuchukua hatua kwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifahamika muda mrefu. Sadiki Mgaya ambaye alishuhudia tukio la kuchomwa kisu na kutolewa macho kwa Said Ally, alisema mtuhumiwa huyo alisema kuwa amekuja kwa ajili ya kulipa kisasi kwa wakabaji baada ya yeye kukabwa.

Alisema baada ya kufanya tukio hilo, askari walifika katika eneo hilo na mtuhumiwa huyo akiwa hapo na wananchi waliwaonesha askari lakini hawakuchukua hatua zozote badala yake waliwataka wananchi wamkamate.

Aidha wananchi hao pia wamemlalamikia Mkuu wa Kituo cha Polisi Mnyamani na kudai kuwa amekuwa akipelekewa taarifa za uhalifu ikiwemo za vibaka lakini mtu anapokamatwa akifika kituoni hapo anatoa rushwa na kuruhusiwa kuondoka.

Lakini akiondoka askari wengine wanatumwa tena kumkamata. Kauli hizo za wananchi zikamfanya Sirro kutoa kauli ambapo alisema askari na maofisa wote ambao wanashindwa kutimiza wajibu wao watachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa kazi.

"Najua wapo askari na maofisa wa ovyo ambao hawajui kutimiza wajibu wao, lakini nikuahidi Mkuu wa Mkoa tutawachukulia hatua, nimesikia hapa wananchi wanalalamika askari wanachukua rushwa, tutachunguza tukijiridhisha basi ni lazima tuchukue hatua," aliongeza.

Aidha Sirro alisema watafanya doria kubwa katika eneo hilo ili kuwakamata wote wanaohusika na matukio ya kihalifu kwani wamebaini katika eneo hilo bado kuna uporaji mdogo mdogo.

"Tutarudi hapa tunaomba ushirikiano wenu bila ninyi kutuambia hatuwezi kujua, nawaomba wazazi muwakanye watoto wenu ambao wanahusika na matukio hayo kwani tutakapoanza msako huo wasije wakalalamika, uhalifu haulipi na mwisho wa siku utamkosa mtoto wako," alisisitiza.

Kwa upande wake Makonda aliwataka wananchi hao kujitolea kufanya ulinzi shirikishi na kuwataka wananchi kuchangia ulinzi huo ili vijana hao wahusike kufanya ulinzi na kulifanya eneo hilo libaki na amani.

"Tuna wajibu wa kufanya ulinzi shirikishi wananchi mtoe michango, hapa Sirro amesema mapungufu yaliyopo kwenye vituo yanafanyiwa kazi, niwaase tu mjiepushe na matukio ya kuhalifu kwani wale watakaokamatwa sheria itachukua mkondo wake," alisema Makonda.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hilo scorpion mngelikamata kabla hajafanya uharifu wa kumtoa mtu macho mnasuburi watu watolewe macho ndiyo mfanye kazi

    ReplyDelete
  2. Kama amekamatwa ni vizuri, sasa ili nayeye aipate ladha ya hayo ayafanyayo, asipelekwe jela kula ugali wa bure, bali atolewe macho yake yote, kisha arudishwe uraiani aendelee na maisha yake..tuone kama ataweze kuendelea kutoa watu macho akiwa hana macho.

    ReplyDelete
  3. Alhamdulillahir Rabbil Alamiin

    ReplyDelete
  4. Mkuu safi sana nimependa comment yako na yeye atolewe macho halafu arejeshwe uraiani

    ReplyDelete
  5. abakwe na jeshi zima mpaka akicheka awe anakunya automatical ilhali akiwa hana jicho hata moja,halafu kila siku awe anakatwa fundo au pingili moja ya kiungo chake ,akianziwa kukatwa pingili za vidole mpa miguu na ..laanatullaah..kitendo alichokifanya ni cha kinyama kisicho na mfano ktk karne hii..kamtoa macho yote mawili noo haiwezekani..haspelekwe jela huyo maisha yake yawe hapo hapo maabusu ili awe punching bag..rangi ya mama nini..hata akiimba azabu kali imuhusu iwe mfano kwa wengine..

    ReplyDelete
  6. Hapa Huyu jizi, jambazi, jiuaji, mtoa macho, chinja chinja vyote yeye, walaaah haina haja ya kulionea huruma jitu katiri kama hili tena dude baya, afadhali hata hayawani wa mwituni kuriko hili, sasa kwa kuwa mwenzake anaitaji macho apate kuona, na yeye ndie alimuharibia, ni hivi, atolewe hili dudumizi, hayawani lililokuwa linajita Scorpion, ili mwenzake apandikizwe apate kuona tena, na lenyewe ndio lisione si ndio lilifanya hayaaaa, chonde chonde Serikali ruhusini huyo dudu limnyama scopion litolewe macho ili mwenzake apandikiziwe macho yake,

    ReplyDelete
  7. Hakika huyu jamaa ni mnyama asiyelingana na mnyama yeyote, hafai kabisa katika dunia hii. Hakika amenikera sana. Unamtoboa macho binaadam mwenzako? Aisee. Huyu jamaa anatakiwa atobolewe macho kabla ya yote kuendeleaa. Inauma sana kwakweli. Harafu wananchi wa Eneo hilo LA buguruni palipotokea hilo tukio ni hivyo kabisa. Yaani mtu anafanya ukatili kama huo wanamuangalia tu. Imeniuma sana. Naomba jeshi lichukuwe hata Kali.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad