Ni kawaida kwa watu maarufu kupewa heshima ya kutoa tuzo kwa kumtangaza mshindi, mshindi wa Big Brother Africa 2014 Idriss Sultan kutokea Tanzania na msanii na mtangazaji wa TV kutoka Angola Weza Solange walipewa heshima ya kutoa tuzo ya kundi bora.
Msanii wa Bongofleva Alikiba kutoka Tanzania, Sauti Sol kutokea Kenya na mrembo Yemi Alade kutokea Nigeria ambaye pia alishinda tuzo ya msanii bora wa kike walikuwa ni miongoni wasanii waliopewa nafasi ya kuperform.
Wasanii kutoka Tanzania wanaounda kundi la Navy Kenzo Aika & Nahreel walikuwa ni baadhi ya watu maarufu waliopewa heshima ya kutoa tuzo za MTV Mama 2016.
Msanii wa Nigeria Wizkid alipopanda kwenye state kuchukua tuzo yake ya msanii bora wa kiume MTV Mama Awards 2016, tuzo ambayo ilikuwa inawaniwa pia na mtanzania Diamond Platnumz.
Jina la mtanzania Diamond Platnumz lilikuwa katika list ya wasanii watakaoperform katika tuzo za MTV Mama 2016, Diamond aliperform wimbo wa Kidogodogo aliowashirikisha P Squre wa Nigeria.
Baada ya baadhi ya wasanii kuperform Partorankig wa Nigeria, Sarkodie wa Ghana, Kored Bello, YCEE na Falz wa Nigeria walikuwa katika list ya wasanii watakaoperform katika tuzo hizo.
Zamu ya utolewaji wa tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana ilikuwa ya msanii wa South Africa DJ Maphorisa akiwa kawashirikisha Wizkid wa Nigeria na DJ Buckz ndio waliofanikiwa kushinda tuzo hiyo ya MTV Mama 2016.
Wizkid hakuishia kushinda tuzo mbili pekee katika usiku huo, lakini waandaaji walikuwa wamemuweka katika list ya wasanii walioperform pamoja na DJ Maphorisa na Emcee.
Msanii Yemi Alade kutoka Nigeria ambaye anafanya vizuri na hit songs zake kadhaa ndio alitangazwa mshindi wa tuzo ya msanii bora wa kike ya MTV Mama 2016.
Baada ya kushinda tuzo ya msanii bora wa kiume kwa mwaka 2016, Wizkid wa Nigeria allitangazwa pia kuwa mshindi wa tuzo ya msanii bora wa mwaka wa tuzo za MTV Mama 2016.
Tanzania safari hii hakuna msanii aliyefanikiwa kushinda tuzo hata moja ya MTV Mama 2016, kwa upande wa tuzo ya Best Breakthrough Act aliyokuwa anawania Rayvanny wa WCB ilichukuliwa na Tekno wa Nigeria wakati tuzo ya chaguo la wasikilizaji iliyokuwa inawaniwa na Yamoto Band ilichukuliwa na Jah Prayzah wa Zimbabwe.
Msanii kutoka United State of America USA Future ndio alikuwa msanii wa mwisho kutoa burudani na kuhitimisha sherehe za utoaji wa tuzo hizo za MTV Mama 2016 kutoka Johannesburg Afrika Kusini.
bora Dai kakosa. watz. tusinge kula wala kunywa leo.
ReplyDeleteSalaam na Babu tale walisahau kuhonga? au walijua wao ni zaidi so Almasi ata win tuu.
ReplyDeleteDiamind ulichemka jana, ile show mbaya cd haikufanya kazi sauti yako imegoma ulipania sana ila Mungu alikufedhehesha. na Zari kampeleka Tiffa kanisani.lol
ReplyDeleteMwenyezi Mungu hamfichi mnafik. mlimzimia Kiba mic. mbona jana Domo sauti ilikuwa mbaya na mkaongeza cd juu. Salaam rudi kwa mganga kamwambie mambo hayakuwa mazuri jana. stupid.
ReplyDeletehe he inachekesha mdau uliyeandika kuwa Salaam na Babu Tale wamesahau kuhonga na kweli safari hii wamesahau pia wamesahau kwenda kwa mganga
ReplyDeleteWIVU WENU TU UNAWASUMBUA JAMANI LOO!!!
ReplyDeleteTENA WATAKUFA MIDOMO WAZI MAANA SIONI NI KWA NINI WANAMSEMA DAI WAKATI NI WATANZANIA WOTE WALIOKOSA TUZO HIZO
Deletehata wewe Anony 9.35 AM. una wivu tena wakunuka bila kidonda! its true Sallaam na Tale wamesahau kuhonga na kufanya ngeli... nani asojua..
ReplyDelete