Mwamuzi Aliyechezesha Mpira wa Yanga na Simba Afungiwa Miaka Miwili..Kadi Nyekundu ya Mkude Yafutwa

Habari zilizoifikia ambazo hazijathibishwa na TFF, Bodo ya ligi wala chama cha waamuzi ni kwamba, mwamuzi wa kati Martin Saanya na msaidizi wake namba moja (line one) Samwel Mpenzu, wamefungiwa miaka miwili kuchezesha soka.

Chanzo chetu kimeitutonya kuwa, uamuzi huo umefikiwa na kamati ya saa 72 iliyokutana kuwajadili wawili hao baada ya kuwepo kwa malalamiko kwenye mechi ya Yanga vs Simba waliyoichezesha Jumamosi October 1.

“Martin Saanya na Samwel Mpenzu wamefungiwa miaka miwili lakini line two Ferdinand Chacha yeye amesalimika,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutoandikwa jina.

“Kadi nyekundu aliyooneshwa Jonas Mkude imefutwa baada ya kamai hiyo kujiridhisha kuwa kadi hiyo ilitolewa kimakosa.”

Baada ya mchezo wa Yanga vs Simba, kuliibuka mijadala mingi na mikubwa juu ya mwamuzi Martin Saanya kulikubali goli la Tambwe ambaye aliushika mpira kabla hajafunga huku Samwel Mpenzu akilaumiwa kwa kulikataa goli la Simba lililofungwa na Ibrahim Ajibu kwa madai alikuwa ameotea kabla ya kufunga.
Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SIMBA,YANGA NI SHIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIDA.
    SIASA NA PESA IKO NDANI YAKE.

    ReplyDelete
  2. Tanzania kwa simba na yanga hata iweje lazima tatizo litakuwepo,labda mtoe mwamuzi kutoka ulaya,

    ReplyDelete
  3. Acheni ushabiki, mpira hauchezewi chumbani, kla kitu kilikuwa wazi na wote tuliona, kasoro katika mchzo wowote ni za kawaida na ninachokiona hapa kuna jazba na hasira zisizo na maana. Kutatua changamoto za michezo kwa nchi yetu linahitaji kuwa makini na kujiongeza zaidi, tusiamuee masualaya michezo kwa mashinikizo. Mfano unapoamua kuzinyima timu mbili za Yanga na Simba kucheza Dar ni busara kweli? hapa ndo kuna uchumi wa timu hizi mbilina mpira unaendeshwa kwa gharama kubwa na unahitaji wapenzi na mashabiki kuingia uwanjani kwa kiingilio. Mwamuzi alikuwa sahihi kwa maamuzi yake, baadhi ya makosa hakuyaona na hasa goli la Tambwe kulingana na beki wawili wa simba walivyokuwa wamesimama na mfungaji wa bao hilo. Goli wanalosema simba lilikuwa halali, halikuwa halali kwani mfungaji kabla ya kufunga aliotea na baada ya kipindi cha kwanza, Azam Tv walianza kuliangalia bao hilo kwa mwendo mnato na kuonyesha mfungaji alikuwa ameotea kabla ya kufunga. Kwa kifupi namshauri mhe, Nappe asingeanza kutoa adhabu aliyoitangaza kwa umma kabla ya vikao vya pande zote mbili hiyo ndiyo busara na wote sisi ni watanzania, uanawafukaza yanga na simba Dar wakachezee wapi? Busara tu itumike katika kutatua kilichotokea na mambo kama haya yametokea duniani na si kuwa ni tukio la kwanza kutokea kidunia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanasemaga kila muwamba ngoma ngozi huvutia kwake.
      Kweli kabisa mfungaji alikuwa ameotea kabla ya kufunga,lakini kila mwanasimba atasema wameonewa ili mradi ushabiki maandazi tu.Tambwe angekuwa ni wa simba bila shaka wangempa kila aina ya sifa ila kwa kuwa yuko yanga ni kilio cha kuonewa,Tambwe ni bonge la mchezaji,anajua kuhadaa mabeki,hakati tamaa,sasa walitaka mara baada ya kugusa mpira asimame asicheze hata kama muamuzi hakupiga filimbi?na jee mbona mabeki wa simba walimfuata nyuma,si wangesimama kuashiria Tambwe hakuwa sawa?Mbaya zaidi viongozi wanaongea na kupiga kelele saana ndani ya simba na yanga, hawajasomea wala kucheza mpira wa miguu .Ukiangalia hata mechi ya simba na Azam kulikuwa na figisu si za kawaida ila kwa kuwa azam hatuna ubishi mara baada ya kipenga cha muamuzi tunakubali tu matokeo.Najua jinsi mchakato ulivyo sidhani kama azam wana nafasi ya kuchukua ubingwa japo ni mapema sana kubashiri,lakini kiukweli natamani simba wachukue ili tuone watafikia wapi kimataifa.Haipendezi kwa simba hasa viongozi wao wanavyoiponda yanga kuwa imebebwa ndio maana hawajafika mbali kimataifa,hivi kwa anaejua mpira na tukiacha ushabiki wa kijinga kweli yanga hawajasogea hata hatua kimataifa?Fujo uwanjani hazizuiliki kwa kuwa hata viongozi wenyewe wanachangia,angalia kwenye suala la kung'oa viti,hivi kweli Viongozi wa simba wanashindwa kuwadhiti waharibifu pamoja na kwamba picha zinaonyesha?ADHABU YA MASHABIKI KUTOINGIA UWANJANI INGESAIDIA

      Delete
  4. HAHAHAHAHAHA!UONEVU!NITAJIENI MUAMUZI AMBAYE HAJAWAHI KULAUMIWA SOKA LA BONGO,HASA AKICHEZESHA YANGA/SIMBA.NANI?MCHEZO UPI?ZAWADI NONO NITATOA.NA NDIO MAANA TUNASHABIKIA TIMU ZA NJE.ADHABU ZIANZIE KWA VIONGOZI.TFF YENYEWE NI U-SIMBA/U-YANGA NA AZAM KIDOGO SANA. NA KAMWE HAKUNA TIMU NYINGINE ZITAWAKILISHA KIMATAIFA ZAIDI YA HIZO TATU.PIA VIONGOZI WA TIMU WAPEWE ADHABU KALI.KIONGOZI ANATANGAZA KWENYE VYOMBO VYA HABARI ATAWAAMBIA MASHABIKI WAFANYE FUJO HALAFU FUJO INATOKEA NA WALA HACHUKULIWI HATUA,KUNA MAADILI HAPO KWELI?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Alichukuliwa hatua Muro kwa kauli kama hizo lakini Manara kalindwa.

      Delete
  5. tatizo ni kwamba hizi kamati za tff za nidhamu au nyingine zinaongozwa na hawa hawa viongozi wa simba na yanga, sasa fikiria KABURU NYANGE ni mwwenyekiti wa kamati ya nidhamu tff na vile vile ni makamu mwenyekiti wa simba, offcourse lazima atalazimisha adhabu kali kwa mwamuzi kutokana na hasira za timu yake kukosa ushindi, na hii imetokea mara kwa mara kwa huyu jamaa kutoa adhabu kali kwa waamuzi wanaochezesha mechi za Yanga, ni upuuzi mtupu! hizi kamati zinatakiwa zisiwe zinaongozwa na viongozi wa hizi timu mbili.

    ReplyDelete
  6. SIMBA WANA KIBURI SANA,NI WAHUNI,TOFAUTI NA TIMU NYINGINE LIKO WAZI.

    ReplyDelete
  7. UMEMUONEA,AU KWA KUWA KABURU NI SIMBA?

    ReplyDelete
    Replies
    1. cyo tu yeye ni simba bali ni MAKAMU MWENYEKITI WA SIMBA!

      Delete
  8. Enter your comment...kama ilvyo kwa malinzi no mpenz wa yanga na mamuzi yk sio

    ReplyDelete
  9. Hii kali na mpya,na ni upuuzi.Mmejiridhishaje mpaka mkaamua kufuta kadi nyekundu?mmesikiaje maneno aliyokuwa anatamka mkude kwa muamuzi,achilia mbali vitendo amavyo kila mtu aliona?

    ReplyDelete
    Replies
    1. ni upumbavu, na cyo upuuzi! yawezekana alimtukana refa! refa nae ni binadamu!

      Delete
  10. Kwakuwa Simba na Yanga wamefungiwa kuchezea uwanja wa taifa, msimu huu FIESTA 2016 iiimmmoooo ndani ya Uwanja wa Taifa................puu!

    ReplyDelete
  11. USHAURI,SIMBA NA YANGA WAKIWA WANACHEZA KIPENGA KIPULIZWE NA MALINZI,WASAIDIZI WAWE MO na MANJI.Moto wake sasa uwiii!
    Hahahahahahhahahhah!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad