'Performance' ya Chris Brown Mombasa Yamchefua Rama Dee

Katika show hiyo, alisindikizwa na wasanii kama Wizkid kutoka Nigeria, Alikiba kutoka Tanzania, Vanessa Mdee kutoka Tanzania na baadhi ya wasanii kutoka nchini Kenya na Uganda.

Katika show hiyo msanii huyo maarufu kutoka Marekani Chris Brown alionekana akiimba kwa kufuatiliza CD yaani 'Playback' na si kufanya muziki 'live' jambo ambalo limemfanya mwanamuziki Rama Dee kutoka Tanzania kuonesha kuwa hakupenda kile alichofanya msanii huyo mkubwa.

Rama Dee kupitia ukurasa wake wa Instagram alindika na kuwataka watu wa Afrika kushtuka kwani yeye hajapendezwa kabisa na kile alichofanya Chris Brown kwenda kuimba kwa kuifuatiliza CD nyuma ili hali inafahamika kuwa yule ni msanii wa kimataifa, hivyo alipaswa kuonesha utofauti mkubwa katika kufanya show.

"Huyu naye kaenda Mombasa kaweka 'CD' kaanza kuimbia juu. Ndiyo msanii wa kimataifa huyu? Tuamke waafrika jamani" aliandika Rama Dee

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na tuamke kikwelikweli hii tabia ya kuwapapatikia hawa wana music wa west tuiache wakati wao wanaiga dancing styles zetu. Na bit zetu.Kama ilivyo Mali Asili zetu zinazalishwa hapa tunawapelekea wao halafu Wanatuuzia sisi wenyewe tena. Basi angalau tusikubali tufanyiwe hivyo na music hebu wa Africa tuwe na pride tuvithamini na kujivunia vitu vyetu.

    ReplyDelete
  2. Na ni kweli wanatukuzwa sana kama hadi wasanii wetu wa Afrika wakifanya nao show za pamoja ndiyo tunasikia hizo habari wamezimiwa mic ili kuwafurahisha wao, inakuwa too much sasa wanapewa attention iliyopitiliza! Ndiyo maana wanaendelea kutudharau kwa sababu sisi wenyewe hatuthaminiani! Kwanza kwa sasa Tanzania tunafanya muziki mzuri sana huko ulaya kwa sasa kawaida sana... Tuthamini vya kwetu...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad