Rais Magufuli Aongoza Kura Kuwania Tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’

Rais John Magufuli anaongoza  kura za kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’, ambayo hutolewa kwa watu walioonyesha mchango kwa jamii.

Huku zikiwa zimebaki siku 21 kwa mshindi wa tuzo hiyo kutangazwa, Rais Magufuli anachuana na Rais wa Mauritius,  Ameenah Gulib;  Mwendesha Mashtaka wa Afrika Kusini, Thuli Madonsela; Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel Le Roux na Taifa la Rwanda.

Mpaka jana jioni, Dk Magufuli alikuwa anaongoza kwa asilimia 75 likifuata Taifa la Rwanda na nafasi ya tatu alikuwa Madonsela wa Afrika Kusini.

Rais Magufuli anayetimiza mwaka mmoja madarakani wiki ijayo, utendaji wake umeonekana kuwagusa wananchi wa kipato cha chini, hasa kwa falsafa yake ya Hapa Kazi, uwajibishaji na mikakati yake ya kubana matumizi ili kuokoa fedha kwa kuzuia sherehe zisizo na tija.

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Akishinda hiyo Tunzo itasaidiaje kubadili hali ya maisha ya watanzania kwa sasa? Wataalam wa uchumi naomba mnasaidie kwa nn uchumi wa nchi unapopanda pesa inaadimika mitaani na kwa nn uchumi wa nchi ukishuka pesa inapatikana kirahisi mitaani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Magu, kAJICHA PESA KWA sPIDI HII NI JAMBO JEMA. Mtoto wetu!! Tukipata kama wewe humu Barani kwetu Watatu wengine. Basi Jua Tutaigawa Afrika katika pande nne na tutakupena kwaq muda maalumu naimani Afrika itakuwa Mpya. Na heshima yake itarudi kama ulivyo rudisha hapa kwetu na m
      Maendeleo ya Haraka sana na Watu Kujitambua na Kuwa Waaninifu uliojawa na Uzalendo... JPJM tunzo hii unasitahiki na haina Mpingamizi.. Viva Afrika Viva CCm ViVa TZ. Viva Magufuli... Aluta Continua... Hapa Kazi Tu. Mtoto wetu wa nyumbani Mwenyewe Siyo Wa kuimport... Mli Mpola Ngosha!! Mwangaluka wawa!!! Mungu Mbariki JPJM na Umpe afya Njema.....

      Delete
  2. OYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
  3. Asante Mungu,Tutakuelewa tu.

    ReplyDelete
  4. NA HILI NALO WATABISHA TU,SUBIRINI MUONE.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwenye-wivu-ajinyonge, lakini-ukweli-utabaki-kuwa-ukweli!!!!!

      Delete
  5. jamani kura zinapigwa wapi??

    ReplyDelete
  6. Huyu ndiye rais tunayemuhitaji watanzania tulio wengi, siyo sisi sasa anaonekana kidunia na Mhe,JPM tuzo hiini yako tu.Najua wapo wengi wanaojua kutumia mitandao hii lakini kwa hili wapo kimya.Rais wa Tanzania ni Dr JOHN POMBE JOSEPH MAGHUFULI, tusubirie 2020. Hongera jembe letu wanyonge. ALUTA CONTINUA.

    ReplyDelete
  7. ACHA KABISA!Wapi bi.Samia?wapi Majaliwa?wapi Mchemba na viongozi wengine?
    Kazeni buti tuko nyuma yenu,hakuna kushindwa.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  8. Ukweli haujifichi. ..na uongozi. Bora. Unahidhirissha Na. Unapongezzwa . Hii Ni alama Na ushahodi tosha kwa wabishina qasiotaka kuelewa ..Habari ndiyo hiyo...Hapa Kazi Tu..mikataba 22 mmeshuhudia maikiri utaabza siku cha che za usoni nq the massive stadium yenye hadhi ya kimataifa inakuja kwa wadoso wa kukata sandenti Jemedari JPJM

    ReplyDelete
  9. Magu, Mtoto wetu!! Tukipata kama wewe humu Barani kwetu Watatu wengine. Basi Jua Tutaigawa Afrika katika pande nne na tutakupena kwaq muda maalumu naimani Afrika itakuwa Mpya. Na heshima yake itarudi kama ulivyo rudisha hapa kwetu na m
    Maendeleo ya Haraka sana na Watu Kujitambua na Kuwa Waaninifu uliojawa na Uzalendo... JPJM tunzo hii unasitahiki na haina Mpingamizi.. Viva Afrika Viva CCm ViVa TZ. Viva Magufuli... Aluta Continua... Hapa Kazi Tu. Mtoto wetu wa nyumbani Mwenyewe Siyo Wa kuimport... Mli Mpola Ngosha!! Mwangaluka wawa!!! Mungu Mbariki JPJM na Umpe afya Njema.....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani weee!!! Acha aliemzaa Huyu ngosha, uzazi wake umebarikiwa

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad