RAIS Magufuli Atafuna Mfupa Uliomtoa Jasho Kikwete

RAIS John Magufuli ameweka rekodi mpya ya kulipa deni la taifa ambayo haikuwahi kufikiwa katika kipindi cha miaka 12 iliyopita.

Katika rekodi yake hiyo mpya, Rais Magufuli amefanikiwa kulipa deni la taifa la ndani na nje ya nchi katika kipindi kifupi cha miezi mitatu kwa kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa na mtangulizi wake, Rais Jakaya Kikwete, katika kipindi chote cha miaka 10 aliyokaa madarakani.

Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya uchumi wa taifa iliyotolewa jana mbele ya waandishi wa habari na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu ofisini kwake Dar es Salaam, Rais Magufuli amelipa shilingi bilioni 99 za deni la ndani na amelipa pia Dola za Marekani milioni 90 za deni la nje kwa muda wa siku 90.

Taarifa hiyo ya Gavana Ndulu inaonyesha kuwa kasi hiyo ya ulipaji deni la taifa kwa fedha za ndani ambalo hivi sasa limefikia shilingi trilioni 51 haijawahi kufikiwa kipindi chote cha Serikali ya awamu ya nne.

“Serikali imelipa Dola za Marekani milioni 90 kwa deni la nje ambazo ni sehemu ya Dola za Marekani bilioni 600 zilizokopwa Benki ya Stanbic na imelipa pia shilingi bilioni 99 za deni la ndani.

“Ninaposema limelipwa si kwamba Serikali haikopi kabisa, hapana, kinachofanyika kwa sasa fedha zinazokopwa ni ndogo kuliko zile zinazolipwa tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

“Utaratibu huo wa ulipaji uliwahi kutokea kati ya mwaka 2003 na 2004 na unaweza kupunguza kasi ya kuongezeka deni la taifa,” alisema Gavana Ndulu.

Katika mkutano huo, Gavana Ndulu alizungumzia pia mwenendo wa ukuaji uchumi kwa nusu mwaka unaoanzia Januari mpaka Juni 2016 kwa kueleza kuwa ukuaji wa pato la taifa umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 5.7 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2015.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu ni mwadilifu na mwaminifu, tatizo wengine bomu tamaa nyingi za kujaza mifuko yao, hasa maraisi wetu wa huku Africa ni corrupt tu, wanachowaza wapate uraisi awe tajiri kwa kuiba hela zinazoingia serikalini au akope mihela huko nje ajifanye matumizi ya nchi kumbe anajaza mifuko yake mpka zinamwagika, sijui hela zote za nini anazijalizia mifukoni mwao Wakati mataifa yao ya Africa dhiki tu imewandama lakini waliowengi hawayaoni hayo, viongozi wengi bara la Africa corrupt, kwa kukopa mihela za kujaza mifukoni mwao, kwa kuweka mikataba ya uongo uongo, kuuza ardhi kwa matajiri, matumizi mabaya ya fedha za kodi ya wananchi wa chini. Yaaani arimladi tu, mpka kunapelekea Taifa kukosoa huduma muhimu, ndio maana tunambiwa IQ zetu ndogo. ( uimara wa akili mdogo ) na hii yote ni sababu ya viongozi wa bara la Africa ndio wanaokwamisha bara hili IQ zao ni ndogo alafu wanangangani uongozi kama wawe maraisi

    ReplyDelete
  2. Taatifa zinaleta uchochezi
    Kwani hali ya uchumi hupanda na kushuka kila leo
    Pamoja na kazi nzuri ya kusimamia uchumi wa nchi hasa kodi
    Tungependa sana huyo mtoa habari za uchumi tuonesheni video akisema haya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmmh ndio wale walala usingizi, Talifa ziko sawa, unadai video hujui kusoma, au ndio wale wakwamishaji? Linakugusa, au tatizo ni shule ufaham mdogo

      Delete
  3. Safi sana pedejee magu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad