Rais Magufuli atimiza ahadi yake kwa Balozi Omben Sefue...Amteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi Chuo cha Diplomasia

Hatimaye Rais John Magufuli ametimiza ahadi yake kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue baada ya kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Diplomasia.

Balozi Sefue amepata uteuzi huo jana ikiwa ni miezi kumi tangu Rais Magufuli atengue uteuzi wake [kama Katibu Mkuu Kiongozi]kwa sababu ambazo hazikutajwa huku akiahidi kumpangia kazi nyingine na nafasi yake ikajazwa na Balozi John Kijazi, .

Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa wizara hiyo, Balozi Augustine Mahiga amewateua wajumbe sita wa Bodi ya chuo hicho cha Diplomasia.

Wajumbe hao ni Balozi Begum Taj, Balozi John Haule, Juma Salum, Profesa Mohamed Bakari, Profesa Innocent Zilihona na Mathias Abias.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza rasmi Oktoba 6 mwaka huu.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. JEMBE!HATA ANA KILANGO APEWE KAZI

    ReplyDelete
  2. Balozi Sefue, Karibu sana Katika Jumu hili ambalo uwezo wako na Umahiri wako Unaridhisha kwa kiwango Cha Juu Kabisa. Ni imani yetu kuwa Utajenga Maadili na kuendeleza Uhamasishaji kwa Vijana wetu ambao tutategemea wanapo tuwakilisha wanakua na Malengo endelevu ya Kuinufaisha nchi na Wananchi katika nafasi zao za utumushi na kuonesha Uvumilivu na Nidhamu ya hali ya Juu. Ili waweze kutoa sura ya nchi yetu huko Ughaibuni katika kudumisha na kuendeleza nchi hii. Imani na wewe tunayo kubwa. Uadilifu wako na umahiri wako ndiyo uliotupa huu msukumo. Karibu sana na tuendele na kuchapa Kazi katika hii awamu yetu ya Hapa Kazi Tuu.

    ReplyDelete
  3. Balozi Sefue, Karibu sana Katika Jumu hili ambalo uwezo wako na Umahiri wako Unaridhisha kwa kiwango Cha Juu Kabisa. Ni imani yetu kuwa Utajenga Maadili na kuendeleza Uhamasishaji kwa Vijana wetu ambao tutategemea wanapo tuwakilisha wanakua na Malengo endelevu ya Kuinufaisha nchi na Wananchi katika nafasi zao za utumushi na kuonesha Uvumilivu na Nidhamu ya hali ya Juu. Ili waweze kutoa sura ya nchi yetu huko Ughaibuni katika kudumisha na kuendeleza nchi hii. Imani na wewe tunayo kubwa. Uadilifu wako na umahiri wako ndiyo uliotupa huu msukumo. Karibu sana na tuendele na kuchapa Kazi katika hii awamu yetu ya Hapa Kazi Tuu.

    ReplyDelete
  4. Balozi Sefue, Karibu sana Katika Jukumu hili ambalo uwezo wako na Umahiri wako Unaridhisha kwa kiwango Cha Juu Kabisa. Ni imani yetu kuwa Utajenga Maadili na kuendeleza Uhamasishaji kwa Vijana wetu ambao tutategemea wanapo tuwakilisha wanakua na Malengo endelevu ya Kuinufaisha nchi na Wananchi katika nafasi zao za utumushi na kuonesha Uvumilivu na Nidhamu ya hali ya Juu. Ili waweze kutoa sura ya nchi yetu huko Ughaibuni katika kudumisha na kuendeleza nchi hii. Imani na wewe tunayo kubwa. Uadilifu wako na umahiri wako ndiyo uliotupa huu msukumo. Karibu sana na tuendele na kuchapa Kazi katika hii awamu yetu ya Hapa Kazi Tuu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad