RAIS Magufuli: Hakuna Fedha za Tetemeko Kwenda Magereza. Wafungwa "Watetemeke" Kujenga Magereza yao

“Katibu Mkuu Kiongozi, hakuna kuwapelekea wafungwa wa Karagwe fedha yoyote, hizi za maafa ya tetemeko. Watetemeke na kufanya kazi,” alisema Rais Magufuli na kuibua kicheko kwa watu waliohudhuria hafla hiyo.

Rais John Magufuli amesema Serikali haitajenga Gereza la Kitengule Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera lililobomoka kwa tetemeko la ardhi, badala yake ameliagiza Jeshi la Magereza liwatumie wafungwa kufanya kazi hiyo.

Alitoa agizo hilo juzi wakati akifunga mazoezi ya kijeshi ambayo kitaalamu yanaitwa ‘amphibious landing’ yaliyofanyika Kijiji cha Baatini, Bagamoyo mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Katika mazoezi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na kushuhudia wanajeshi wakilikomboa eneo lililotekwa na maadui ukanda wa majini, Rais Magufuli alimtaka Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kutopeleka fedha za maafa kujenga gereza hilo

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

  1. Tetemeko likiharibu ikulu na yeye aijenge ikulu
    Jino kwa jino
    Magereza hayajengwi ovyo
    Kuna ulinzi ambao wafungwa hawapaswi kujuwa
    Tunaropoka sana awamu ya Tano

    ReplyDelete
  2. Sio kujenga gereza lao tu, wajenge hata madaraja huku wakisimamiwa na makandarasi,wanakula ugali wa bure tu.......

    ReplyDelete
  3. Nafikiri Ph.D. Ya pombe inatia
    Wasi wasi nimesoma mtandaoni
    Fyuu
    Bora ya Msoga za kupewa
    Anaropoka na kukurupuka bila kufikiri
    Ni mtoto mdogo
    1959
    Watu wazima wanamuogopa kwa lipi
    CCM fyuuuuuuuuh

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad