Sababu ya Rais Magufuli Kutishia Kumfukuza Kazi Mtoto wa Dada yake

Rais Dkt John Pombe Magufuli ametishia kufukuza kazi mtoto wa dada yake kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutopeleka umeme katika kiwanda kipya cha kusindika matunda cha Bakhresa.

Rais Magufuli alisema jana alipokuwa akifungua rasmi kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa kilichopo Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani.

Wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi, kiongozi mmoja wa kiwanda hicho akieleza changamoto wanazokumbana nazo alisema kuwa tatizo la umeme ambapo wameongea na TANESCO lakini hadi leo umeme haijafikishwa kiwandani hapo hivyo kuwalazimu kutumia jenereta kuendesha mitambo kitu kinachopelekea kuongezeka kwa gharama za uzalishaji.

Aliposimama kuhutubia Rais Magufuli aliuliza kama kuna kiongozi yeyote wa TANESCO mkoa wa Pwani ndipo akasimama mtoto wa dada yake. Rais Magufuli akamwambia anafahamu kuwa amefanya kazi nzuri alipokuwa Kagera na Tanga na kuwa anataka ahakikishe umeme unafika katika kiwanda hicho la si hivyo ataanza kumtumbua yeye ambaye ni mtoto wa dada yake.

Rais Magufuli alielekeza maswali mawili kwa TANESCO wakati wa hotuba yake, kwanza, kama TANESCO wanania ya kufanya biashara, kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo kwa sababu ni fursa ya kibiashara, pili aliuliza kama TANESCO wanania ya kuona Tanzania inakuwa ya viwanda, kama wanania, kwanini hawapeleki umeme kiwandani hapo.

Rais Magufuli ametoa miezi miwili kwa TANESCO kuhakikisha kuwa wanafikisha umeme kiwandani hapo kama wanataka kuendelea na kazi zao.

Kuhusu ombi la uongozi wa kiwanda hicho kutumia  gesi asilia inayopita jirani na kiwanda hicho, Rais Magufuli alisema kuwa watakaa na Wizara ni Nishati na Madini na Wizara ya Viwanda na Biashara kuona namna wanaweza kulishughulikia hilo.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hili jembe tulipe hata miula minne atawale

    ReplyDelete
  2. This is a Man of Action, JPJM hata ucheleweshaji katika Maendeleo ya Nchi. Na kwa Muonekano Huu.. Ameweza Kutoa Onyo na Kudhihirisha kuwa Kazi Ni Kazi na Tunataka Performance driven Cadre in All Areas. Urafiki, Undugu / Ujamaa / Mtoto wa Mjomba/ Mtoto wa Shangazi... Haito ileta Tanzania Yetu Mpya. Tunachotaka ni Uzalendo / Uaminifu / Uwajibikaji na Ufanisi wa hali ya Juu katika utendaji. Prof Muhongo pia alisisitiza kuwa Mteja asitufate sisi kumpa umeme bali ni sisi kuwaqfata wateja na kuhakikisha tunawafungia umeme na will evaluate the perfomance on achievment. Sasa Hili la Mh JPJM lime clear beyond doubt. kuwa You dont perform. you are out hata kama ni mwanangu!! Kwa hiyo Watendaji tushirikiane kumsaidia Baba JPJM .. Nia yake inaonekana na Lengo lake linajulikana.. Ni Mimi Na wewe kushirikiana nae katika kuileta Taanzania yetu mpya.. Ukiona na Kuisikiliza ile Hotuba tuliyo hudhuria Bandarini .. Ni moja kwa moja JPJM hataki ucheleweshaji na Hangoji taarifa Ofisini au Kudelegate mtu au watu. He makes timely decision na Draws an Action plan with Authority. The next time he wants things are positively done. MUNGU AKUPE UMURI NA aFYA.. tUKO BEGA KWA BEGA .. yOU sTYLE IS uNIQUE. the game changer in African Leadership.. Karibu sana Dodoma Magu. Nidhamu na ufanisi Umeurudisha kwa kiasi kikubwa..Mungu akujaalie kila la kheri na akulinde na kila Shari. Sandenyi Jemedari nilimdodo wa kukaya..Hapa Kazi TU

    ReplyDelete
  3. This is a Man of Action, JPJM hata ucheleweshaji katika Maendeleo ya Nchi. Na kwa Muonekano Huu.. Ameweza Kutoa Onyo na Kudhihirisha kuwa Kazi Ni Kazi na Tunataka Performance driven Cadre in All Areas. Urafiki, Undugu / Ujamaa / Mtoto wa Mjomba/ Mtoto wa Shangazi... Haito ileta Tanzania Yetu Mpya. Tunachotaka ni Uzalendo / Uaminifu / Uwajibikaji na Ufanisi wa hali ya Juu katika utendaji. Prof Muhongo pia alisisitiza kuwa Mteja asitufate sisi kumpa umeme bali ni sisi kuwaqfata wateja na kuhakikisha tunawafungia umeme na will evaluate the perfomance on achievment. Sasa Hili la Mh JPJM lime clear beyond doubt. kuwa You dont perform. you are out hata kama ni mwanangu!! Kwa hiyo Watendaji tushirikiane kumsaidia Baba JPJM .. Nia yake inaonekana na Lengo lake linajulikana.. Ni Mimi Na wewe kushirikiana nae katika kuileta Taanzania yetu mpya.. Ukiona na Kuisikiliza ile Hotuba tuliyo hudhuria Bandarini .. Ni moja kwa moja JPJM hataki ucheleweshaji na Hangoji taarifa Ofisini au Kudelegate mtu au watu. He makes timely decision na Draws an Action plan with Authority. The next time he wants things are positively done. MUNGU AKUPE UMURI NA aFYA.. tUKO BEGA KWA BEGA .. yOU sTYLE IS uNIQUE. the game changer in African Leadership.. Karibu sana Dodoma Magu. Nidhamu na ufanisi Umeurudisha kwa kiasi kikubwa..Mungu akujaalie kila la kheri na akulinde na kila Shari. Sandenyi Jemedari nilimdodo wa kukaya..Hapa Kazi TU

    ReplyDelete
  4. Mr President, You deserve to rule this country. for 3 decades . we need to submit the motion of extra ordinary peoples request. Ikibidi Mh. Ndugai na Dada Tulia tumepeleke referendum nchi nzima.. TUNAMTAKA MAGU ASHIKE NCHI MPAKA INYOOKE NA WATANZANIA TUJITAMBUE.. ELIMU MFUMO UNABADILISHWA MATUNDA YAKE NI BAADA YA MIAKA 20 AU 25. MAGU MUNGU AKUPE AFYA NA SUBIRA NA UMURI TAWILE. NCHI HII WEWE UTAIWEZA NA NI KWELI HUMUONEI HAYA MTU CHA UKWELI HUKIFICHI NA MSG UNAZISEND VERY CLEAR NA DELIVERED. HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  5. JPJM, Tunamshukuru Mungu kutuletea wewe kuishika Nchi yetu. Kiutendaji / Kimaadili / Kiufanisi / na inadhirisha na kuonesha jinsi ulivyo uchukia Ubadhirifu / Misheni Town / Dili dili na Hewa Hewa.. Tunaona jinsi mabadiliko na unyeyekevu katika shughuli za serikali na umma. hivi sasa wafanyakazi wako maofisini na watuhudumia bila kuuliza senti sivyo kama hapo awali unawekewa vizingiti katika kila jambo na la kumalizika leo utachukua mwezi kama siyo miwili. Spidi yako ni nzuri na kama ulivyo tuahidi huto tuangusha.. TUNAONA SASA. UNAWANYOOSHA NA WANAELEKEA... HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  6. JPJM, Tunamshukuru Mungu kutuletea wewe kuishika Nchi yetu. Kiutendaji / Kimaadili / Kiufanisi / na inadhirisha na kuonesha jinsi ulivyo uchukia Ubadhirifu / Misheni Town / Dili dili na Hewa Hewa.. Tunaona jinsi mabadiliko na unyeyekevu katika shughuli za serikali na umma. hivi sasa wafanyakazi wako maofisini na watuhudumia bila kuuliza senti sivyo kama hapo awali unawekewa vizingiti katika kila jambo na la kumalizika leo utachukua mwezi kama siyo miwili. Spidi yako ni nzuri na kama ulivyo tuahidi huto tuangusha.. TUNAONA SASA. UNAWANYOOSHA NA WANAELEKEA... HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  7. Damu nzito kuliko maji
    Poleni kina kilango hamkupewa hata onyo mkatbuliwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, Hapo umechamganya Kiudaku mauwio hayapo hapo. Kwa hii tabia yako . I reccomend you kwenda Melelani utatajirika.

      Delete
    2. huutaki utajiri? unaweza kununua Noah

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad