Samatta alitokea benchi na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa 2-0

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta katika mchezo wake wa jana alitokea benchi na kuisaidia timu yake, KRC Genk kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao ya Hispania katika mchezo wa Kundi F Europa League Uwanja wa Laminus Arena, Genk.


Katika mchezo huo anbao Samatta aliingia dakika ya 56 kumbadili kiungo Mbelgiji Thomas Buffel, mabao yote ya Genk yalifungwa na mabeki, Jakub Brabec kutoka Jamhuri ya Czech la kwanza dakika ya 40 na Mnigeria Onyinye Wilfred Ndidi la pili dakika ya 83.


Kwa matokeo hayo, Genk ambayo ililazimishwa sare ya
2-2 katika mchezo wake uliopita na Royal Excel Mouscron Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja Stade Le Canonnier mjini Mouscron sasa inagongoza Kundi F kwa kjufikisha pointi sita baada ya mechi tatu, ikishinda mbili na kufungwa moja.

Huo unakuwa mchezo wa 28 kwa Samatta tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 10 msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.

Katika mechi hizo, ni 14 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tatu msimu huu, wakati 13 alitokea benchi nane msimu uliopita na 10 msimu huu – na mechi tisa hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad