Dar es Salaam, Oktoba 9, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza kuzindua shindano la DJ bora ambalo linalenga kuibua na kukuza vipaji katika sekta ya muziki na burudani nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shindano hilo jijini Dar es Salaam, Mkrugenzi wa Mawasiliano wa Serengeti John Wanyancha alisema kuwa shindano hilo limedhaminiwa na bia inayozalishwa na kampuni hiyo Smirnof Black Ice, na wakati huo huo ikimaanisha kuwapatia mashabiki wa muziki fursa ya kufurahia vibao vya muziki vya hivi karibuni vitakavyochezeshwa na ma-DJ walio na vipaji vikubwa.
Kwa mujibu wa Wanyancha, Smirnof Black Ice ni chapa inayoongoza katika vighezo vya bia iliyotayari kunyweka ikiwa ni maarufu mioongoni mwa wanywaji wa tabaka la kati katika maeneo yote ya mjini na vijijini.
“Tunaamini kwamba kupitia shindano hili SBL itawapa wakati mzuri wapenzi wa muziki watakaokuwa wanatembelera baa wakati tukitoa fursa maridhawa ya kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji katika ulimwengu wa muziki na ma-DJ.
Mkurugenzi huyo aliyataja majiji ambayo yatakuwa wenyeji wa matukio na idadi ya ma-DJ watakaotoa burudani katika mabaa kwenye mabano kuwa ni Dar es Salaam (20), Dodoma (4), Arusha (5), Morogoro (4), na Mwanza (5). Shindani hilo linaanza mwezi huu wa Oktoba na litadumu hadi Desemba.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa hadhira inayolengwa katika mashindano hayo ni vijana walio na umri kati ya miaka 18 hadi 30 na kufafanua kuwa burudani hiyo inawafaa sana wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu pamoja na vija walio na weledi.
“Itakuwepo zawadi nono kwa ma-DJ watakaoshinda,” alisema na kubainisha kwamba zawadi hizo zitajumuisha seti ya vifaa vya kuchanganya muziki, kompyuta mpakato na mashine kuchanganya muziki kwa washindi watatu watakaoingia fainali.
“Tunatoa wito kwa ma-DJ wote, wasimamizi wa baa na wapenzi wa muziki katika majiji haya kushiriki kwa wingi katika shindano hili la kuvutia ili kufurahia na burudani inayotolewa na sekta ya muziki nchini Tanzania,” alisema Wanyancha.
MWISHO