Taasisi na Mashirika ya Umma nchini yametakiwa kujiendesha kwa faida huku yakiwa na mtazamo wa kiushindani na makampuni yaliyo chini ya sekta binafsi na kwamba hakuna sababu yoyote kwa mashirika hayo kuendeshwa kwa hasara na kugeuka mzigo kwa serikal
Msajili wa Hazina nchini Bw. Lawrence Mafuru ametoa agizo hilo jana jijini Dar es Salaam wakati akisaini makubaliano ya kiutendaji na taasisi 12 za umma, mkataba unaohusisha malengo ya uendeshaji, namna ya kuhudumia wananchi sambamba na usimamizi bora wa rasilimali za umma zilizopo ndani ya mashirika hayo.
Zoezi hilo la linafanya idadi ya taasisi ambazo msajili wa hazina amesaini nazo makubaliano kufikia thelathini tangu aanze utaratibu huo unaoendana na falsafa ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji katika taasisi na mashirika ya umma.
Katika maelezo yake Bw. Mafuru amesema haikubaliki kuona makampuni na taasisi za umma zikiendelea kupata hasara kwa kutekeleza majukumu yale yale ambayo taasisi na makampuni binafsi yanapata ufanisi na faida pasipo visingizio vyovyote.
HAPA KAZI TU
ReplyDeleteA New Era .. in African leadership being lead With Our Honorable President JPJM.
ReplyDeleteFocusing on Performance and Achievement. You do not achieve your out. Hongera Mafuru. Haya ndiyo tunayo yataka Tanzania yetu Mpya. Focus in customer satisfaction / Quality product / A Vision to next level / Respect / Competitive and Fair Price. Logistical sound with on time delivery..( All With Plan B strategy) .... Hapa Kazi tu