Singeli ni Muziki wa Kihuni, Hautodumu – Juma Nature

Singeli ni muziki ulioibuka kwa kasi na kujizolea mashabiki lukuki na kufanikiwa kuzalisha vipaji kadhaa.

Licha ya kuonekana kufanya vizuri mpaka kufikia kiasi cha kuwashawishi wasanii wa muziki mwingine kujiingiza katika muziki huo, wapo baadhi ya watu wameonekana kutokuwa na imani nao.

Nilifanikiwa kupiga story na msanii mkongwe wa Bongo Flava, Juma Nature, mapema wiki hii katika studio zake za Halisi Records kuhusu muziki huo ambapo yeye alidai kuwa Singeli ni muziki ambao hautoishi kwa muda mrefu bali unapita tu kwasababu ni muziki wa kihuni.

“Singeli itapita tu kwasababu ya uhuni,” alisema. “Unajua raia wengi wa Bongo hawapendi mambo ya kipumb*vu pumb*vu na mashabiki wetu wengi sana sio wahuni ila wahuni wanakuja katika hizi section, so wakija kwenye section hapo muziki hakuna tena,” alisema Nature ambaye hivi karibuni aliachia ngoma yake mpya iitwayo Mtumba.

By Edward Fabian

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KWELI KABISA,NA NDIO MAANA SINGELI INABAMBA SANA MITAA YA USWAHILINI AMBAKO WAHUNI NDIO WENGI.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad