Sumaye: Sirudi CCM hata waninyang’anye Mashamba Yangu Yote

Siku moja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kutangaza nia ya Serikali kumnyang’anya shamba Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, mwanasiasa huyo mkongwe amedai hilo halimtikisi.

Sumaye ambaye tayari ameshakabidhiwa notisi ya siku 90 kutokana na kutoliendeleza, amesema kuwa tayari suala hilo ameshaliwasilisha mahakamani na kwamba mwanasheria wake ndiye anayefahamu tarehe iliyopangiwa kesi hiyo.

“Nilienda mahakamani na ikaamuriwa kusiwe na shughuli yoyote, nasubiri tarehe ya kesi ambayo mwanasheria wangu ndiyo anaijua,” Sumaye anakaririwana MwanahalisiOnline.

Mwanasiasa huyo aliyehamia Chadema miezi michache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, amesema kuwa kama CCM wanataka kumdhoofisha kwa kumnyang’anya mashamba ili arejee haitawezekana.

“Kama walidhani kwa kunifanyia hivi nitarudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasahau, hata kama nilikuwa na nia hiyo sirudi,” amesema Sumaye.

Serikali imetangaza kuanza mchakato wa kumnyang’anya Sumaye shamba lake lililoko Mwabwepande jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa ameshindwa kuliendeleza kwa muda mrefu, kinyume na matakwa ya sheria.

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sheria IPO miaka yote.sasa mahakama itapingana Na Sheri ya ardhi?endeleza uone kama watakugusa.Hii ni zama nyingine hakuna kuoneana aibu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sanaa tu, zile zama za kuoneana na kukandamizana na kufanyana watumwa na watwana zimeishaa,

      Delete
  2. Sumaye Fediliki, Wewe huyu!! MCC sidhani kama watakutaka hata kama ukiwaomba. Lakini hebu tuambie arizi na siasa wapi na wapi?? au ndiyo kavile wanavyofanya wale wa NCH na dani la kodi ya Mjengo... Ama kweli bora ufilisike mfukoni na hii spidi kuliko kufilisika Kichwani... Hovyo uliendaga shule?? Na umuri wako ni miaka mingapi kwa sasa... Nasikia ulikuwa mgonjwa Pole sana Mungu atakuafu . ila kumbuka Hapa ni Kazi Tu....

    ReplyDelete
  3. Sumaye Fediliki, Wewe huyu!! MCC sidhani kama watakutaka hata kama ukiwaomba. Lakini hebu tuambie arizi na siasa wapi na wapi?? au ndiyo kavile wanavyofanya wale wa NCH na dani la kodi ya Mjengo... Ama kweli bora ufilisike mfukoni na hii spidi kuliko kufilisika Kichwani... Hovyo uliendaga shule?? Na umuri wako ni miaka mingapi kwa sasa... Nasikia ulikuwa mgonjwa Pole sana Mungu atakuafu . ila kumbuka Hapa ni Kazi Tu....

    ReplyDelete
  4. Mimi sio CCM. Ila ardhi isiyoendelezwa inachukuliwa sio siasa. Upanga huo uwapitie viongozi wote wanaopakatia ardhi kubwa, viwanja nk bila kuendeleza. Isiwe Sumaye tu.

    ReplyDelete
  5. Shangilieni tu sababu imemkuta sumaye aliyetoka ccm nankuingia ukombozini sasa taratibu kama mchwa mtaona familia zenu zinavyopukutika maana mnavyoambiwa madawa hakuna mnashangilia,uchumi umeshuka mnashangilia,ajira hakuna mnashangilia,watanzania wana hali mnaya mnashangilia maana mnapenda porojo za majukwaani mnapenda kusikia wenye navyo wanakomeshwa kumbe hamjui wapiganapo tembo nyasi ndio huumia.watanzania mnatia huruma sana kudhangilia hata vifo vyenu na future mbaya za watoto zenu..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nawe Una yako, hayo madawa na hizo ajili zilikuwepo, enzi za Huyu mpka na zama za 10 period zilizopita si hivi hivi tu katika hii Tanzania, tena afadhadhali ya zama hizi, watu unaona hata kuwajibika wanawajibika, huko nyuma zama hizo zilikuwa zinaongoza kwa ubadhilifu wa Mali za umma, ufisadi uliopitiliza, mpka ukasababisha Kila kitu kwenda holela holela, Elimu shida, afya shida Kila siku madaktari wamegoma hakuna vitendea kazi, watu wachache na hao wanaojita wanasiasa wakaona wao ndio wenye hii nchi, kungendelea vile kungezunga masikini na tajiri, watu wachache Elite, hiii ni mbaya na hatari kwa mustakabali wa Taifa na uchumi wake pia

      Delete
  6. tuna vijana wa kileo hatukuhitaji tunataka Damu change tumeshamalizana na wewe WE DONE

    ReplyDelete
  7. Tatizo mlitegemea uji wa mgonjwa mkasahau akipona mnakufa na akifa mnakufa pia, badilikeni

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad