Lakini si kwa Miss Tanzania 2016, Diana Edward aliyevishwa taji Jumamosi hii, jijini Mwanza. Tangu ameanza kushiriki shindano hilo katika hatua za vitongoji, mrembo huyo alikuwa amejianda kuwa Miss Tanzania.
Diana mwenye asili ya kimasai, kwa muda wote wa ushiriki wa shindano hilo, aliuweka mbele utamaduni wake, kitu ambacho ni nadra kwa Mamiss wengine ambao wengi wao wamekulia mjini.
Amekuwa akijihusisha na shughuli za utetezi wa masuala ya kijamii, hasa watu wanaoishi mazingira magumu, pamoja na kampeni za kutokemeza ukeketaji. Wiki moja iliyopita alitoa documentary fupi kuhusu ukeketaji unaofanyika katika jamii yake ya kimasai. Yeye mwenyewe ni mhusika. Video:
Kwa Video hiyo tu Tayari kashakua miss world hata kama hatashika nafasi ya kwanza lakini Ulimwengu usha mjua...nikazi ngumu sana na Mataifa mengi yana pinga vita ukeketaji....Milango isha Funguka masai galy acha wakupige vita ila Mungu yu pamoja nawe keep it up.
ReplyDelete