Tetesi za Hemed PHD Kutoka Kimapenzi na Mwigizaji Tausi...Tausi Afunguka

Muigizaji na mchekeshaji kwenye tasnia ya Bongo Movie, Tausi, amesema hana mahusiano yeyote nje ya kazi na Hemed PHD huku akisema huwa wanakutana kambini na hana hata namba ya simu ya msanii huyo.

Tausi ameibuka na kusema hivyo baada ya kuwepo uvumi wa kujimwaga na staa huyo ambapo aliiambia eNewz “Hemedy ni msanii mwenzangu tu na nilipokuwa nyumbani nilikuwa namuona tu kwenye TV na mara ya kwanza nilipokutanishwa naye na meneja wangu Lamata ilikuwa ngumu hata kuongea naye na nilitetemeka saana na nilikuwa mwoga saana”

Mbali na hilo, Tausi, alizungumza kuhusiana na wavulana ambao wamekuwa wakitamani kuwa naye huku wakijiuliza wataishi vipi na yeye akisema hakuna jambo ambalo haliwezekani kwani hata yeye ana ndoto za kuishi na mwanaume na kuwa na watoto wasiopungua 12.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tausi umetisha Mama!! Ni Poa tu. Hakuna cha Ajabu. kama imetoka ndivyo hivyo mamake alikuwa Anakumaindi sana. na ikibidi mnahalalisha.

    ReplyDelete
  2. Lkn shoga usiwe na wazo la kuzaa watoto wengi hivyo nafkiri watatu au wawili ni tosha Dada

    ReplyDelete
  3. Tausi dada nimekupenda na pia napenda kazi zako mwenyezi Mungu atakujalia ndoto yako ya kuzaa watoto 12

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad