TIMU ya Vijana Serengeti Boys Yashindwa Kufuzu Fainali za Africa

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys imeshindwa kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika nchini Madagascar mwaka 2017 baada ya kupoteza mchezo wake wa mwisho wa kufuzu dhidi ya Congo Brazzaville kwa kufungwa bao 1-0 ugenini.

Bao pekee katika mchezo huo limefungwa dakika za mwisho katika mchezo huo na kuzima ndoto za watanzania kuisuhudia timu yao ikienda kuliwakisha taifa kwenye michuano mikubwa barani Afrika.

Kocha wa Serengeti Boys Bakari Shime amesema matokeo hayo huenda ni mipango ya Mungu licha ya wao pia kuwa na mipango yao kuhakikisha timu inafuzu kwenye mashindano ya AFCON.

“Ni ngumu hata kuelezea, kimsingi tulifanya kilakitu kizuri na tulifanikiwa kwa kilakitu, game tuliikamata lakini kosa dogo ambalo tumelifdanya wenzetu wakalitumia na kutumaliza. Vijana walicheza vizuri sana hawajawahi kucheza kama walivyocheza leo”.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam, Serengeti Boys ilishinda kwa magoli 3-2, hivyo kuruhusu goli 1-0 ugenini kunafanya matokeo ya jumla kuwa 3-3 lakini Tanzania inatupwa nje kwa sheria ya goli la ugenini.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Poleni,na ni yetu sote,Lakini ndio wimbo kwenye soka la TZ kwa sasa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad