CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Serikali kuhakiki akaunti na mali za Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT) na wenzake waliokuwa katika kamati za fedha za Bunge, ili kubaini kama zinalingana na kipato walichokuwa wakipata.
Msemaji wa chama hicho, Christopher Ole Sendeka, amesema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari, akimuhusisha Kiongozi huyo Mkuu wa ACT na tuhuma za ufisadi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
”Nilikuwa najiuliza hivi chuki ya Zitto kwa Serikali ya Awamu ya Tano, inayopambana na mafisadi imetoka wapi wakati yeye alikuwa anasimamia mashirika hayo.
“Miongoni mwa taasisi hizo alizokuwa akisimamia na baadhi ya marafiki zake ndiyo hao walionunua hekari moja kwa Sh milioni 800, wakati ilikuwa ikiuzwa kwa Sh milioni 25 na walikuwa wamejificha kwa maslahi binafsi,” alisema katika ofisi ndogo za Makao Makuu, Lumumba Dar es Salaam.
NSSF ndiyo iliyonunua hekari 20,000 Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Sh milioni 800 kwa kila hekari, badala ya Sh milioni 25 na kujikuta katika hatari ya kupoteza Sh bilioni 270, katika mradi wa ujenzi wa mji wa kisasa wa Dege Eco Village.
Kutokana na tuhuma hizo za NSSF zilizoibuka upya katika kamati ya PAC wiki hii, Sendeka alisema ni vema Serikali ikague kuona kama akaunti za viongozi wa zamani wa kamati hizo, maisha yao na mali walizonazo, zinafanana na mapato halali waliyokuwa wakilipwa.
Alisema alikuwa anaangalia msukumo wa ghafla na mapenzi ya akina Zitto waliyokuwa wanayapata kwa nchi, kumbe ilikuwa ni kichaka cha kuficha baadhi ya maswahiba zao wasichukuliwe hatua.
Aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina nia ya kurudi nyuma katika jambo lolote na kuwa itasonga mbele huku akiamini kuwa Serikali iliyochaguliwa na watu haiwezi kufa.
“Tunahakika Serikali ya Magufuli iliyopata ridhaa ya kutumikia watu, haitafutika kwa kelele za mlango wa baadhi ya makuwadi na watu waliolipwa kuchafua taswira ya Tanzania,” alisema.
Aliongeza kuwa Serikali hiyo itaendelea kushughulikia wakwepa kodi pamoja na kuchunguza mambo aliyoanzisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa bandarini.
Kauli ya Zitto
Akizungumzia tuhuma hizo, Zitto Kabwe alisema hana muda wa kujibu alichoita kuwa ni porojo na vioja vya Sendeka.
Alifafanua kuwa CCM ni chama dola na kuna taasisi nyingi za uchunguzi za Serikali, ikiwemo Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai (DPP) na kushangaa kwa nini vyombo hivyo havisemi, aseme Sendeka?
Ufisadi NSSF: CCM Yataka Akaunti za Zitto Kabwe Zipekuliwe.
4
October 29, 2016
Tags
Atueleze sisi Wananchi kama kweli kipato chake na mali zake zinalingana na kile kipato alichokuwa anakipata. Aache ngiliba zake za kutudanganydanganya sisi Wananchi wa kawaida.
ReplyDeleteAlipata utajiri wa ghafla utadhani ulishushwa,mweh!
ReplyDeleteMh.Zitto,tunaamini wewe ni kiongozi bora na hasa baada ya kufichua uhalifu uliokuwa unalitafuna taifa,kwani kuna ubaya gani ukatoa au kueleza chanzo cha mapato yako?Fanya hivyo kiongozi kuliko kuanza kulumbana na Ole Sendeka.
ReplyDeleteZitto Kabwe. Kwa Nia ya kukunyamazisha ukafanya DILI. Wewe Zitto bila ya haya wala kuona vibaya ukaingia Dili na ukala pesa za salama hoi. Zitakutokra puani..hatutolifumbia macho wala masikio..wanaume wanaingua kazini na Tutakushughulikia HUNGRY FACE..KILAZA.hapa hauli Mali yetu jitayarishe kurudisha kabla mambo hayaja cha-cha ..JPJM Na Kassimu wameuchukia Ubadhirifu na ujanjs WA kinyonga..haulipi ..Aluta continua..
ReplyDelete