Walimu Waipa Serikali Siku 15 Ilipe Madeni Yao

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimetoa siku 15 kwa Serikali kumaliza madai yao ya muda mrefu vinginevyo watachukua maamuzi magumu.

Rais wa CWT, Gratian Mukoba amesema kuwa uvumilivu wao umeelekea kufikia ukingoni kwani wamekuwa wakikaa mezani na Serikali mara kwa mara na kupewa ahadi za kutatua matatizo yao lakini hadi sasa hazijatekelezwa.

Alisema kuwa Agosti  22 na 23 mwaka huu, Baraza la chama hicho cha walimu lilipitisha maazimio kupitia kikao chake, maazimio ambayo yalisainiwa pia na upande wa Serikali kwa ahadi kuwa wangeyafanyia kazi lakini imeendelea kuwa kimya.

“Siku chache baadae tuliambiwa tusubiri mchakato wa kuhakiki watumishi ukamilike. Lakini licha ya mchakato huo kukamilika Serikali imeendelea kukaa Kimya,” Mukoba anakaririwa na Tanzania Daima.

Aliyataja madai hayo kuwa ni pamoja na posho ya madaraka kwa wakuu wa shule, muundo wa madaraka, walimu kutopandishwa madaraja na kulipa madeni ya walimu.

“Ninachoweza kukwambia ni kwamba mwishoni mwa Oktoba ambao umebakiza siku 15 tutachukua uamuzi mzito ambao haujawahi kutokea na hatutaki lawakama kutoka sehemu yoyote ile,” alisema Mukoba.

Rais huyo wa CWT alidai kuwa ingawa Serikali imepiga hatua katika sera ya elimu bure na madawati, lakini mazingira ya walimu na ufundishaji yameendelea kuwa magumu hivyo ni vigumu kupandisha ubora wa elimu.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hamna nguvu walimu
    Njooni wote ukuta kiji magu
    Kitaufyata NGUVU YA SHUKRANI

    "Katika maisha yangu siwezi kusahau mchango mkubwa wa Mzee Ali Hassan Mwinyi. Mzee Mwinyi akiwa Mwenyekiti wa CCM ndiye alisimamia kikao cha Chama kilichoniteua mimi kwa mara ya kwanza kugombea Ubunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki mwaka 1995. Kama Mzee Mwinyi angekata jina langu siku ile, huenda leo mimi nisingekuwa hapa. Nakushuruku sana Mzee wangu Mwinyi maana huo ulikuwa ndiyo mwanzo wa safari yangu ya uongozi. Pili, ninamshukuru pia Mzee Benjamini William Mkapa ambaye aliniteua kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi mwaka 1995 mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge. Mwaka 2000 akiwa Mwenyekiti wa CCM aliniteua kugombea Ubunge na nilipochaguliwa alinifanya kuwa Waziri kamili wa ujenzi hadi mwaka 2005. Nashukuru kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kugombea Ubunge na kuniteua kwa nafasi ya Uwaziri tena bado nikiwa na umri mdogo. Mzee Mkapa ahsante sana.

    Ninamshukuru Mzee Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye aliendelea kunilea katika uongozi kwa kuniteua kuwa Waziri wa Wizara mbalimbali, ikiwemo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi pamoja na Wizara ya Ujenzi. Kwa Mzee Kikwete mbali ya kupitisha jina langu kugombea Ubunge wakati akiwa Mwenyekiti wa CCM mwaka 2010 aliamua kujitishwa mzigo, mzito wa kusimamia mchakato wote wa kumpata Mgombea Urais 2015, akaniamini hadi kuteuliwa na mikutano husika ya CCM. Kwa Mzee Kikwete pia nimejifunza mambo mengi lakini kubwa zaidi ni uvumilivu na ustamilivu. Nasema kwa dhati kabisa kuwa Mzee huyu ni mvumilivu na mstamilivu sana. Ni viongozi wachache wenye uvumilivu na ustahimilivu wa namna hii. Binafsi sina cha kumlipa zaidi ya kutoa ahadi ya kufanya kazi kwa bidii ili kumuenzi." - Rais John Pombe Magufuli (Mkutano Mkuu wa CCM, Dodoma julai 23, 2016)


    ReplyDelete
  2. Gratia Mukoba, Unacho zungumza tunakielewa na Serikari katika ngazi zote inalitambua hili suala. Na hata Mh. Majaliwa analifahamu. Kazi linafanyiwa na Ufumbuzi upo. Subira Huvuta kheri. Tunawaomba muendeleee hivyo na hivi karibuni mtaona matunda yake. Japo kuwa itakuwa kwa awamu awamu ..Hapa Kazi Tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad