Wanakijiji Mvumi -Chamwino Wachoma Moto Gari na Kuuwa Maafisa wa Taasisi ya Kilimo

Wakuu kuna habari zinasambaa mitandaoni kuwa kuna Maafisa wa Taasisi ya Kilimo ya Seliani iliyopo Mkoani Arusha wameuawa na wanakijiji wa Mvumi.

Kukatokea kutokuelewana kati ya maafisa hao na wanakijiji,kiasi cha maafisa hao kuchomwa moto wao na gari lao. Picha zinatisha.

Wanakijiji wa Mvumi Wilaya ya Chamwino ndio wamechoma gari ya serikali na kuchoma maafisa wa serikali wakiwa ktk majukumu yao.

Watu 35 tayari mbaroni wakiwemo viongozi wa kijiji.

Waziri wa mambo ya ndani aliposema ugaidi haijaingia tanzania, hii maana yake nini? Ama magaidi wanatoka maeneo gani hasa?

Gaidi huzaliwa ndani ya nchi husika. Sasa tukio hili ni ugaidi tosha. Usisubiri alshabab ama bokoharamu, matukio kama haya ni ugaidi tosha.

Note picha za waliochomwa zinatisha sana
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad