Wasanii Acheni Kuandikia Nyimbo Studio - Crazy GK

Msanii King Crazy GK amesema kitendo cha wasanii kuandikia nyimbo studio na kuingiza sauti hapo hapo kurekodi, ni moja sababu inayofanya muziki wa sasa kutoishi kama ule wa zamani.

Akizungumza na East Africa Radio, King Crazy Gk amesema msanii kurekodi wimbo huku akiwa anasoma mashairi kwenye karatasi aliyoandikia inapoteza 'focus' ya msanii na kupoteza hisia.

"Artist hawafanyi mazoezi waanze kufanya mazoezi, waache kuandikia studio, unaweza ukaandikia studio ukaenda nyumbani ukafanya mazoezi, ukishaushika muziki kchwani ndio utaweza kutoa feelings, lakini ukiwa unaingiza muziki unasoma karatasi, unakuwa sio muziki unakuwa muziki wa siku mbili, kwa sababu feelings, mawazo yote na tension yote yapo kwenye karatasi, huwezi kuexpress feelings, kwa hiyo utakuta muziki wa Bob Marley na wa sasa hivi unaoimbwa, wa Bob Marley una maana", alisema Crazy GK.

Pia Crazy GK amesema kitendo cha kuongezeka kwa producers nacho kimechangia kuua ubora wa muziki, kwani wamekuwa wakifanya kazi bila kufuata misingi ya kazi na kuangali msanii wa kweli.

"Siku za nyuma maproducer walikuwa wachache kwa hiyo artist kupata nafasi ilikuwa ni ngumu lazima awe artist wa kweli, kwa hiyo mtu asiyekuwa artist asingepata nafasi, kwa mfano producer alikuwa mmoja Bony Luv au Master Jay, kila mtu anachagua, sasa hivi kila mtu ni producer, watu hawafuati ethics ya sanaa, anaingiza sauti bila kujali viwango mtu kapeleka, ndio maana muziki unakuwa big G", alisema King Crazy GK.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad