Wastani wa Kiasi Cha Fedha Ambacho Mwanamuziki Diamond Huingiza Kwa Siku

Maneno mengi sana yamesemwa kuhusu kiasi cha fedha analichonacho Naseeb Abdul a.k.a Diamondo Platnumz na vile vile unaweza kumuita Chibu Dangote au Baba Tiffah, na wengine kufikia hatua ya kusema anaweza kuwa ndiye msanii tajiri Afrika Mashariki kwa sasa.

Inasemekana kwamba, kwa kuangalia yote anayoyafanya msanii huyo unaweza kuwa na mwanga kiasi fulani wa kujua anaingiza kiasi gani.

Diamond Platnumz, kwa siku anaingiza wastani wa Sh. milioni 20 kutokana na kupakuliwa kwa nyimbo zake zilizoko kwenye mitandao: Kumbuka hii ni pembeni kabisa na shows anazofanya au malipo anayopokea kutoka kwenye makapuni anayoyafanyia matangazo kama Vodacom, Red Gold na NMB.

Na mpaka hapo utaamini sasa ule usemi wake wa siku zote kwamba muziki ni biashara! Na wasanii wengine hawana budi kumuiga Diamond Platnumz, wawe na wivu wa maendeleo na sio kutamani kumshusha alipo sasa.

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. muongo huyo Diamond haingizi milioni 20 kwa siku, mbona amekuwa muongo namna hiyo, kwanza kadanganya kuwa nyumba ni yake kule South africa kumbe si nyumba yake sasa hivi oo naingiza milioni 20 kwa siku, do you kiding me?

    ReplyDelete
    Replies
    1. watu wanalipwa apewe kiki amekua kama Kim Kardashian wa bongo.

      Delete
    2. wewe Anonymous 5:42, Diamond halipwi milioni 20 kwa siku huo ndiyo ukweli

      Delete
  2. Je serikali anailipa ngapi kwenye tax maana 20m ni nyingi kwa siku ndio maana bi zari amekunganganiaaaaa

    ReplyDelete
  3. Simpendi mtoto huyu kwa uongo
    Mtoto wa mtaani utamjuwa tu
    Hata akiwa tajiri

    ReplyDelete
  4. Basi wakweli ninyi anaingiza shilingi ngapi

    ReplyDelete
  5. 20,000,000/- x siku 30(mwezi1) = 600,000,000/- x mwaka 1 (miez 12) = 3,600,000,000/- yan Bilion 3.6 kwa mwaka!!!!!!? hell no. this can not be serious nasema sio kweli yaan sio kweli kabisaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwa hesabu hizi, yaonyesha ni uongo hapati kiasi hiki kwa siku, au mwandishi kakosea ni milioni mbili 2000000 kwa siku?

      Delete
  6. mbona sielewi ni diamond mwenyewe kasema kuwa anapata m20 kwa siku???

    ReplyDelete
  7. Huenda ndiyo maama Zari kaganda hata kusahahu watato wake wa kwanza; fweza siyo mchezo. Ila mara nyingi jamaa huyu huwa hasemi ukweli, kwani aliwahi kusema ana nyumba SA kama miezi mitano iliyopita lakini ni majuzi tu ndipo akasema amenunua nyumba na kuonyesha picha zake, mwezi wa nane alitoa tamko kuwa birthday party ya binti yake inakuja nyumbani lakini mpaka leo haikuwahi kufanyika, na pia baada ya ziara yake ya ulaya alisema kuna reality show ya familia yake imekamilika itatoka hivi karibuni kwenye luninga, lakini mpaka leo hatujaiona. Kwa hiyo maneno ya Diamond ni ya kuchukua kwa makini sana, kwani mengi huwa hayana ukweli; ikiwa ni pamoja na yale ya "Project"

    ReplyDelete
  8. huyo Diamond ni msanii na maneno yake ni ya kisanii, yaani ni kupuuza kila kitu anachosema maana hamna ukweli na maneno anayosema

    ReplyDelete
  9. hivi watanzania mbona hamjiongezi? kwani hapo lipi la ajabu??? utube zinalipa sana hasa ukiwa na nyimbo ambazo zinatazamwa sana na ajua jinsi gani ya kufanya biashara. mtakalia wivu mwisho wa siku jamaa anakamata mpunga na mambo yake yanamyookea

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad