Zitto Atoa Neno Ugomvi wa RC Arusha na Godbless Lema

Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameamua kutoa ya moyoni kufuatia hali iliyojitokeza jana mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto. Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alisema kuwa eneo la hospitali hiyo lilitolewa na familia ya Nyaga Mawalla, jambo ambalo wananchi walilipinga wakishirikiana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) na kuzua sintofahamu kama inavyoonekana katika video hii….


Zitto kupitia akaunti yake ya Facebook ameandika hivi;
“Nakasirishwa sana kuona viongozi vijana wanafanya mambo ya hovyo. Mkuu wa Mkoa wa Arusha mdogo wangu Mrisho Gambo una dhamana zaidi Kwa vijana. Mnapofanya mambo ya kijinga mnaharibu nafasi ya vijana kuaminiwa zaidi. Kaa Na Mbunge Godbless Lema mnywe kahawa pale New Arusha Na muanze upya. Ndugu yangu Lema nashauri punguza munkari. Juhudi zako Arusha haziwezi kufutika kirahisi. Nakushauri kaa chini Na Mkuu wa Mkoa wako mpige mstari muanze Kazi upya Kwa pamoja.
Viongozi jiepusheni kuonyesha hasira zenu hadharani. Sio hekima.”
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli Lema pale ulikosea,wakati mwingine hakuna haja ya kuonyesha hisia zako hasa mbele ya kadamnasi kama vile mlivyofanya.Kama Wananchi wote walipinga kitendo cha Gambo,Lema wewe kama kiongozi hukutakiwa kuwaunga mkono wananchi,ulitakiwa kuwasihi na kwamba baada ya pale mngeita mkutano na kuliongelea hilo.Kusema ukweli Kwa hili mmekosa adabu mbele ya wageni,na sijui mwanao akifanya hivyo mbele ya wageni,hata kama ni haki yake unajisikiaje.TANZANIA KWANZA!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sijaona kosa la Lema. Kwa sababu Gambo alimuona Lema lakini aliamua kumdharau na kusema uongo mbele yake, hata mimi nisingekubali. Hivi unaamini kwamba wangeruhusiwa kuitisha mkutano kujadili ama kupinga hotuba ya Gambo? Alichokifanya Lema ni sawa ili siku nyingine iwe fundisho kwa wanaokubali kutumika bila kujali maslahi ya wananchi.

      Delete
  2. ZITO NI RAIS MTARAJIWA KUTOKA VYAMA PINZANI,NA SIO HAO WAKINA.....,MTAKE MSITAKE.MUDA UTAFIKA TU.

    ReplyDelete
  3. KUSEMA KWELI LEMA ALIPASWA KUTUMIA BUSARA ZAIDI. HATA KAMA JAMAA ALIKUA NA KOSA ALITAKIWA KUTUMIA BUSARA. ANGALIA SASA AMEONEKANA BUSARA NI ZERO

    ReplyDelete
  4. Viongozi wa mikoa wachaguliwe kutoka mikoa hiyo.Raisi asiteue watu kumfanyia matakwa yake .vibaya zaidi ccm iache kutumia cheo cha ukuu wa mkoa kwa manufaa ya kichama. Ni lazima mkuu wa mkoa awe mzoefu na anayefahamu mazingira halisi ya kazi zake na kusaidiana na wananchi kuleta maendeleo halisi na si kunitanirisha wenyewe au wakuu waliowachagua

    ReplyDelete
  5. Ninani atakaye vumilia kusikia mtu mzima akidanganya watu!!

    ReplyDelete
  6. ni wazo nzuri wajishushe waongee mmetumwa kuwatumikia wananchi mambo yenu binafsi wekeni kando namuomba Mungu awasafishe vinywa muongee muelewane

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad